• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA yaanza kufungua barabara mpya za vijijini Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: March 1st, 2023

WAKALA wa barabara za mijini na vijijini Tanzania(Tarura)wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,imeanza kufungua barabara mpya zinazounganisha  vijiji vya pembezoni na mji wa Tunduru ili kuwawezesha wananchi kusafiri na wakulima kusafirisha mazao yao kwa urahisi kutoka shambani hadi sokoni.

Barabara hizo zinatajwa zinakwenda kuhamasisha uzalishaji,kuongeza thamani ya mazao na kipato kwa wakulima na kuchochea kukua kwa uchumi wa wilaya ya Tunduru,mkoa wa Ruvuma na Taifa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa TARURA wilayani Tunduru Msola Julius,wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara mpya yenye urefu wa km 3.5 inayounganisha kijiji cha Kidugalo kata ya Mchangani na  katikati ya mji wa Tunduru.

Alisema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Tarura imetenga shilingi milioni 100 kutoka mfuko wa barabara kwa ajili ya kuifungua barabara hiyo ambayo awali haikuweza kupitika kwa urahisi kutokana na kuwa na makorongo na mabonde.

Alisema,kwa muda mrefu wananchi wa Kidugalo hawakuwa na mawasiliano ya barabara ya uhakika,lakini sasa serikali kupitia wakala wa barabara za mjini na vijijini(Tarura)imeanza  mpango wa kufungua barabara mpya na kufanya matengenezo barabara za zamani ili kutoa fursa kwa wananchi wazitumie katika shughuli zao za kila siku.

Aidha alisema,kwa muda mrefu wilaya ya Tunduru ilikuwa na changamoto ya barabara za uhakika ,lakini baada ya kuanzishwa kwa Tarura miaka minne iliyopita na tangu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipoingia madarasani barabara nyingi  katika wilaya hiyo zimefunguliwa na kutengenezwa.

Mwenyekiti wa kitongoji  B cha Mchangani kata ya Mchangani Hausi Bilal alieleza kuwa,awali barabara hiyo haikuweza kupitika kwa urahisi kutokana na ubovu,badala yake wananchi walilazimika kutumia usafiri wa baiskeli tu na wakulima kubeba mazao kichwani.

Alisema,hali hiyo ilisababisha wananchi hasa wa kijiji cha Kidugalo kusafiri kwa shida kwenda maeneo mengine ya wilaya ya Tunduru kufuata huduma mbalimbali za kijamii na wakulima kushindwa kupeleka mazao yao sokoni kwa wakati.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kidugalo hususani wakulima, wameishukuru Tarura kuanza matengenezo ya barabara hiyo ambayo ni tegemeo kubwa kwao kwa ajili ya kusafirisha mazao kufika sokoni.

Dastan Msilasi mkazi wa mtaa wa Mkwanda alisema,matengenezo ya barabara ya Mchangani-Kidugalo imemaliza kilio cha muda mrefu cha mawasiliano ya uhakika na kuipongeza serikali kuitengea  Tarura fedha za kutosha kwa ajili ya matengenezo barabara hiyo.

Ali Yusufu alisema,mawasiliano kati ya kijiji cha Kidugalo na maeneo mengine ya mji wa Tunduru hayakuwepo baada ya kukatika kwa barabara,lakini tangu Tarura ilipoanza matengenezo takribani siku tatu zilizopita  wananchi  wameanza kunufika na wakulima wataitumia barabara hiyo kuuza na kusafirisha mazao yao kwa wakati muafaka.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.