• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TIMU ya Tunduru korosho yapokelewa kibabe

Imewekwa kuanzia tarehe: September 17th, 2023

MKUU wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amewataka wachezaji wa Timu ya Tunduru Korosho kutobweteka  na mafanikio waliyoyapata, badala yake waongeze bidi ya mazoezi ili wafanye vizuri katika mashindano ya Ligi daraja la Pili Taifa.

Mtatiro ametoa kauli hiyo jana wakati  wa mapokezi ya Timu hiyo katika viwanja vya Baraza la Idd Mjini Tunduru yaliyohudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji wa Tunduru mara baada ya Timu hiyo kuwasili ikitokea Kigoma katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa.

Mtatiro ambaye ni mlezi wa Timu  ya Tunduru Korosho alisema, baada ya kuwa mabingwa wa Ligi ya mabingwa wa mikoa, Timu hiyo inahitaji maandalizi ya uhakika sana  ili kujiweka fiti kwa ushiriki wa ligi daraja la pili Taifa ambapo itakutana na Timu nyingine zenye uwezo  mkubwa.

Aidha mlezi huyo amehaidi kuboresha maslahi ya wachezaji,benchi la ufundi pamoja na timu mzima kwa kulipa mishahara fedha zitakazotokana na michango ya wananchi wa Tunduru hususani kutokana na fedha za korosho ambazo kila mwananchi atalazimika kuchangia.

Sambamba na hilo Mtatiro amewataka wananchi kufahamu kuwa TImu hiyo ni wananchi wote wa Tunduru,hivyo wanapaswa kuiunga mkono kwa kuchangia fedha ili iweze kujiendesha na kufanya vizuri katika mashindano yajayo ya LIgi daraja la pili Taifa.

Katika hatua nyingine  mkuu wa wilaya amesema, kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi  watahakikisha wanaufanyia ukarabati mkubwa Uwanja wa michezo wa CCM wilaya unaotumika kwa ajili ya michezo mbalimbali ya mpira wa miguu ili uwe bora na utumike kwa ajili ya ligi inayokuja.

Alisema, ukarabati wa uwanja huo utafanyika kabla ya kuanza kwa Ligi Daraja la pili ambapo Timu ya Tunduru Korosho itashiriki baada ya kuibuka mabingwa wa ,Ligi ya Mabingwa Taifa mashindano yaliyozishirikisha Timu 8 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Kwa upande wake,mwenyekiti wa Timu ya Tunduru Korosho Mohamed Kiyonjo amewashukuru wakazi wa mji wa Tunduru kwa kujitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo na kusema kuwa hali hiyo imeleta hamasa kwa wachezaji  wa timu hiyo kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.

Kiyonjo alisema, ni faraja kubwa kuona idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza kuipongeza na kuipokea timu yao ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wana Tunduru kuendelea kuiunga mkono Timu ili iweze kufanya vizuri zaidi katika michezo yake.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.