Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ruvuma imepiga hatua kubwa katika kuongeza idadi ya wafanyabiashara wanaojiandikisha na kulipa kodi kwa hiari.
TRA wameongeza makusanyo ya mapato kupitia mikakati madhubuti ya utoaji wa elimu ya kodi.
Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Walipakodi, Hilary Gerald, mafanikio hayo yametokana na juhudi za kuimarisha mahusiano na walipakodi kupitia semina, vikao vya ushauri na ushirikishwaji wa viongozi wa kijamii.
Gerald amesema TRA imeweka kipaumbele katika kuwaelimisha wakulima na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari, hali ambayo imechochea mwitikio chanya kutoka kwa walengwa.
Amebainisha kuwa elimu hiyo imeongeza uelewa wa wajibu wa kulipa kodi na kuchochea uzalendo wa kulipa kodi miongoni mwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
Kwa mujibu wa TRA, malipo ya awamu ya pili ya kodi yanapaswa kufanyika kabla ya tarehe 31 Mei, huku mwisho rasmi wa malipo hayo ukiwa ni tarehe 30 Juni, 2025.
Amesema maafisa wa TRA wamepelekwa katika maeneo ya biashara kutoa huduma za makadirio ya kodi, na walipakodi wametakiwa kuwasilisha ritani zao kwa wakati ili kuepuka adhabu.
Gerald amelitaja la lengo la TRA kuwa ni kuhakikisha kila mfanyabiashara anashiriki ipasavyo katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia ulipaji wa kodi kwa hiari.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.