• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TUME ya Rais ya maboresho ya kodi yaifikia Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: February 8th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed,  amesema mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya uwekezaji ambavyo vinaweza kuwa vyanzo vikubwa vya mapato zikiwemo sekta za madini, kilimo na biashara.

Amesema hayo wakati akifungua kikao cha Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na Wafanyabiasha na Wadau Mbalimbali wa Kodi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

"Tuna sekta ya madini, kilimo, biashara, uvuvi, mifugo, tunao wakulima, wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa na vyanzo vingine mbalimbali ambavyo vinachangia pato la taifa, pia maendeleo ya mkoa wetu,"alisema Kanali Ahmed.

Ameongeza kuwa Kodi sio jambo linalompendeza kila mtu lakini endapo wananchi watatengenezewa mazingira mazuri na kuitambua vizuri wanaweza kuwa wadau wazuri wa kulipa Kodi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maboresho ya Kodi nchini, Balozi Maimuna Tarishi, amesema tume hiyo iliundwa kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo ambazo zinahusisha mfumo wa kodi nchini ikiwemo wingi wa kodi, uwepo wa mamlaka nyingi za ukussanyaji kodi pamoja na ukadiria wa kodi.

Amesema tume hiyo inapokea maoni na mapendekezo kutoka kwa walipaji kodi kote nchini ambayo yatawasaidia kuchakata taarifa zote zilizokusanywa ili kupata mfumo bora na ambao wamekubaliana kwa pamoja kwa sababu itakuwa ni sehemu ya maoni yao.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, mapendekezo yanayotolewa yanalenga sheria zinazohitaji kufanyiwa maboresho, mapungufu ya usimamizi wa ukusanyaji kodi, changamoto za urasimishaji biashara hivyo mwananchi ili aweze kulipa kodi ni lazima awe na mazingira rafiki ya kufanya biashara na kuwezeshwa katika uzalishaji.

Wananchi wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maboresho ya kodi ambayo yatapokelewa na Tume hiyo kupitia Dodoso: https://edodoso.gov.go.tz/544978, Simu (Whatsapp na SMS): 0748 755 677, 0738 588 813, 0682 288 784 pamoja  na Baruapepe: maboresho.kodi@gmail.com.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.