Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. SImon Kemori Chaha ,amewaongoza mamia ya wananchi wa Wilaya ya Tunduru kwenye mkesha wa maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, uliofanyika katika viwanja vya Baraza la Idd vilivyopo mjini Tunduru Tunduru.
Mkesha huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, chama , viongozi wa Dini pamoja na wananchi kutoka sehemu mbalimbali wilayani humo.
Wananchi hao walipata fursa ya kusikiliza na kuangalia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan,iliyohusiana na Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.
Kila mwaka Aprili 26 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaadhimisha siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.