MNADA wa kwanza katika zao la ufuta umefanyika katika kijiji cha Lukumbule Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ambapo jumla ya kilo 857,977.70 za ufuta zimeuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Taarifa ya Idara ya Ushirika Wilaya ya Tunduru inaeleza kuwa katika mnada huo kampuni 14 zilishindanishwa ambapo kampuni tatu zilishinda kwa bei ya kilo moja ya ufuta kuuzwa kwa bei ya wastani shilingi 3,822 kwa kilo.
Wakulima Wilaya ya Tunduru wameipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umeleta tija kubwa kwa wakulima
Hivi karibuni wakulima wa ufuta katika kijiji cha Lisimonji Wilaya ya Namtumbo wameuza kilo moja ya ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa shilingi 4,105
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.