Uboreshaji wa bandari ya Ndumbi ziwa Nyasa Mkoani Ruvuma umeleta muitikio mkubwa katika ongezeko la mizigo asilimia 167.83 na Abiria asilimia 175.57 kwa kutumia usafiri wa majini.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Kutokana maboresho makubwa ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani, yamegharimu kiasi cha fedha bilioni 12.2.
Ameongeza kuwa maboresha hayo, yamewezesha kusafirisha shehena ya tani 30,265.12 za mizingo ambapo ni ongezeko la tani 18,965.12 sawa na asilimia 167.83 na abiria 51,531 ni ongezeko la abiria 32,831 sawa na ongezeko la asilimia 175.57.
“Lengo la uboreshaji huo ni kutaka kukuza uchumi wa mikoa inayozunguka ziwa na mamlaka inasimamia katika kuendesha Meli mbili za mizingo na Meli moja ya abiria na mzigo’’,amesema Kanali Thomas.
Hata hivyo, amesema hivi sasa mzigo mkubwa unaohudumiwa ni (gypsum) unaosafirishwa kutokea Bandari ya Mbambabay hadi bandari ya Kiwira na kuelekea nchini Malawi kupitia njia ya barabara.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Meli ya MV Mbeya II ina uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo kwamba Meli hiyo inaendelea kutoa huduma ya usafirishaji ndani ya Ziwa Nyasa kupitia banadari zote 15 kuanzia Mbambabay mkoani Ruvuma hadi Kiwira mkoani Mbeya.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Oktoba 16,2023
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.