• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UBUNIFU wa kufundisha wanafunzi kwa kutumia mapambo,wawashangaza wengi Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: July 11th, 2021

WADAU wa Elimu Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamempongeza Mwalimu Fidea Mapunda wa shule ya msingi Pambazuko kutokana na ubunifu wake wa kufundisha wanafunzi kupitia mapambo.

Pongezi hizo zimetolewa na wadau hao katika hafla fupi ya kutambulisha mradi unaojulikana kama Elimu ya watoto nyumbani uliobuniwa na Mwalimu huyo.Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Heritage Cottage mjini Songea na kushirikisha baadhi ya walimu,waratibu Elimu Kata  na wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Meya wa Manispaa ya Songea Jeremia Kilembe amesema kuwa Mwalimu huyo anastahili pongezi kutokana na ubunifu wake wa kufundisha wanafunzi kwa njia ya mapambo kwa kutumia vitambaa vya kwenye makochi vilivyofumwa kwa mchoro wa ramani ya Afrika,Tanzania  na alama za Bendera ya taifa.

Kilembe amesema kuwa ubunifu uliofanywa na Mwalimu Fidea  utasaidia kuwajengea uwezo watoto na wanafunzi wa kufahamu vitu wakiwa nyumbani badala ya kusubiri mpaka wanapokwenda kuanza shule ya chekechea na msingi.

Mmoja wa mwanafunzi wa shule ya Msingi Taifa Foundation  mjini Songea Gloria Swila amesema kuwa kutokana na ubunifu wa Mwalimu huyo,umeweza kumjengea uwezo wa kuwajua wanyama wakali,wapole,alama ya Bendera ya Taifa,ramani ya Afrika na Tanzania kupitia mapambo.

“Nawaomba wazazi na walezi kuwatengenezea mazingira ya kielimu nyumbani watoto wao kwa kuwaandalia mapambo yanayoonesha wanyama wakali,wanyama rafiki,mapambo yenye rangi ya Bendera ya Taifa na vifaa vinavyotengenezwa kutokana na rasilimali ya miti’’,alisisitiza Gloria.

Naye Kaimu Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Songea Gerald Chavallah amempongeza Mwalimu Fidea kwa ubunifu wake na kuwataka walimu wengine kuiga mfano huo ili ujuzi huo uweze kutumika katika kuwafundisha watoto na wanafunzi wa shule mbalimbali katika manispaa ya Songea.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo Mwalimu Fidea Mapunda amelitaja lengo la kuanzisha mradi huo kuwa ni kwa ajili ya kumuandaa mtoto kupata elimu kupitia mapambo akiwa nyumbani.

“katika kukabiliana na Ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia mtoto anapaswa kuwekewa mazingira wezeshi ya kujifunzia kupitia mapambo ya ndani kwa kufuma vitambaa vyenye picha ya wanyama wakali,wanyama rafiki,rangi za Bendera ya taifa,ramani ya Tanzania,ramani ya Afrika na kutengeneza vitu vinavyotokana na rasilimali za mit’’,alisisitiza.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Julai 10,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.