UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUFANYIKA NOVEMBA,27,2024.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amebainisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 27 mwaka huu.
Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kutoa Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 ambalo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara 145 na 146 inaelezea uwepo wa Serikali za Mitaa ukilenga kupeleka madaraka kwa wananchi.
Uchaguzi wa mwisho wa Serikali za Mitaa ulifanyika Novemba 2019.
Alisema viongozi wanaochaguliwa katika ngazi hizi ni wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa kamati za mitaa na wenyeviti wa vitongoji.
Mchengerwa ametoa tangazo la uchanguzi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 ibara 4(1-3) (Matangazo ya Serikali Na. 571, 572, 573 na 574) ya mwaka 2024.
“Hivyo ninautangazia umma wa Watanzania na vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuwa tarehe 27 Novemba, 2024 itakuwa ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara.”
“Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni. Hivyo ninawatakia uchaguzi mwema, amani na utulivu katika kipindi chote cha uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni, upigaji kura, wakati wa kutangaza na kupokea matokeo ya uchaguzi.”
Aidha, Mchengerwa alisema utauzie wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Vituo utafanyika Septemba 19 hadi 25 mwaka huu, wakati uandikishwaji wa wapigakura utafanyika kati ya Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu.
Alisema uteuzi wa wagombea utafanyika Novemba 8 mwaka huu wakati kampenzi zimepangwa kuanza Novemba 20 hadi 26 mwaka huu.
Alisema alisema wagombea wa nafasi za uongozi watatakiwa kuwa wanachama na wadhamininiwa wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu.
“Mgombea au mtu aliyeomba kuteuliwa anaweza kuweka pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea.”
Mchengerwa alisema nafasi zote zinazogombewa zilikuwa na uongozi kwa kipindi cha miaka mitano na viongozi walioko madarakani uongozi waon utakoma siku saba kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombea uongozi.
“Pia kura zitapigwa katika namna itakayozingatia usiri na kwa kutumia karatasi maalum za kupigia kura ambazo zitatakiwa kutumbukizwa katika masanduku maalum ya kupigia kura.”
Hata hivyo vyama 18 kati ya 19 vyenye usajili wa kudumu vimeshiriki hafla hiyo na kukabidhiwa kanuni za uchanguzi ispokuwa Chadema ambao hawakuwa na mwakilishi
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Juma Ali Khatibu alisema vyama vya siasa vitashiriki uchanguzi huo na kusisitiza kuwa uchaguzi uwe huru na wa haki.
“Tunaomba watendaji wahakikishe uchaguzi huu unakuwa huru na wa haki na usiache migogoro baada ya matokeo. Baraza halitegemei kuona migogoro baada ya Uchaguzi kwani kuna maisha mengine yanatakiwa kuendelea baada ya uchaguzi.”
Pia alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuja na 4R na kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani na kufanya maandamano.
Awali, Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Martin Shigella alisema ushiriki wa Viongozi wa vyama vya siasa katika mchakato wa leo unakwenda kuongeza hari, hamasa kwa wananchi kushiriki katika uchaguzi na kusisitiza kuwa Serikali imekuwa na ushirikiano mzuri na viongozi wa vyama vya siasa ngazi za mikoa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.