WAGENI 22 kutoka sekondari ya Mwanakwereke C Zanzibar wapo mkoani Ruvuma kwa ziara ya mafunzo na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo mkoani Ruvuma.
Wageni hao wamesema wamekuja Mkoa wa Ruvuma kutembela vivutio mbalimbali vya utalii ikiwa sehemu ya mapumziko kila ifikapo mwishoni mwa mwaka kwenda kutalii kwa lengo la kujifunza historia mbalimbali kota mikoa mingine
Akizungumza kwa niaba ya wezake Mwalimu wa sekondari ya Mwanakwereke C, Riziki Chamda Haji. amesema safari hii wamekuja mkoani Ruvuma kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo mkoani umo kwani wanataka kuzifahamu mila na tamaduni vilevile na Historia ya Majimaji
Mwalimu Riziki Amesema safari yao mkoani Ruvuma wameifurahia sana kwani wamepokelewa vizuri toka siku ya kwanza imewafanya wajione wapo sehemu nzuri kwani itasaidia sana wao pindi wakirudi Zanzibar kuhadithia vivutio vilivyopo Mkoani Ruvuma
“Tumefurahi kuja Ruvuma kwani ni mara ya kwanza kuja Mkoa huu asa la zaidi mapokezi ya wenyeji wetu hilo ndio jambo kubwa sana ambalo kama watanzania inapaswa kulienzi kutoka kwa wahasisi wa taifa letu” amesema Mwl Riziki
Hayo ameyasema wataki walipo tembelea chanzo cha Mto Ruvuma pamoja na Pango ambalo lilitumika na mababu kujificha enzi ya vita vya Majimaji lililopo kwenye Mlima Matogoro katika Mji wa Manispaa ya Songea
“Leo hii tumeanza ziara yetu kwa kuja kupanda Mlima wa Matogoro na tumefurahia sana ingawa ni mrefu ila tumejitahidi kufika hadi kileleni mwa mlima wengi wetu ni watu wazima kidogo hatukuhishindwa safari mpaka tumefika juu ya kilima”amesema Mwalimu Riziki
Amesema ukarimu huu uzidi kudumu kwani wao wakirudi wataelezea wengine ili waje wajione maajabu ya mwenyezi mungu katika kuiumba dunia bila shaka itazidi kuimalisha utalii wandani
Naye Mratibu wa Sarafi kutoka Chuo cha Ualimu Songea Marcelino Mganwa amesema ujio wa wageni hao walianza nao mawasiliano nao toka mwezi wa nne mwaka huu walitaka kuja Ruvuma na hili nikundi la tatu kuja kutembelea vivutio vyetu vya utalii
“Tumewakaribisha vizuri sana wageni wetu pia tumewaandalia ratiba nzuri tu ya kutembelea vivutio vyote kwa Mkoa wa Ruvuma leo tumeanza na Mlima matogoro lakini kimsingi ratiba yetu ni kufika mpaka nyasa”amesema Mganwa
Pia ameuomba uongozi wa mkoa na wadau wa utalii mkoani Ruvuma kuanda matamasha mbalimbali ya utalii kwani kupitia matamasha hayo kama mkoa utaweza kuingiza mapato mengi na kuleta tija kwa taifa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.