• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UPUNGUFU wa maji mjini Tunduru kubakia historia

Imewekwa kuanzia tarehe: February 18th, 2024

SERIKALI kupitia Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,imetenga zaidi ya Sh.milioni 80 kwa ajili ya kuchimba visima vinne vya maji ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa mji wa Tunduru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya  hiyo Chiza Marando ameyataja ,miongoni mwa maeneo ya kuchimba visima ni soko kuu la Azimio,soko la Nanjoka,kituo kikuu cha mabasi na maeneo mingine yanayotumika kupakia na kushushua watu wanaotoka pembezoni mwa mji wa Tunduru.

Marando amesema ,wameamua kuchimba visima hivyo katika maeneo tofauti  yenye uhitaji wa maji na kwamba maji hayo yataingizwa kwenye mfumo wa mabomba kabla ya kusambazwa  wananchi .

“Halmashauri tumeamua kushirikiana na Mamlaka ya Maji mjini Tundur (TUUWASA ) ili kuhakikisha wanapunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika mji wa Tunduru”,alisema.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema ,maji hayo yatauzwa na kuwa sehemu ya chanzo cha mapato ya Halmashauri.

Marando,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa magari ya kuchimba visima vya maji kwa kila mkoa hapa nchini na amewaomba wananchi kushirikiana na serikali yao katika ulinzi wa visima na miundombinu ya maji itakakayojengwa katika maeneo mbalimbali.

Msimamizi wa uchimbaji visima kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Kanda ya Kusini Thomas Masheyo amesema ,utafiti unaonesha kuwa eneo kubwa la mji wa Tunduru  lina maji mengi ambayo yanatosheleza mahitaji ya watu wa mji huo.

Ameshauri wananchi wanaotaka kuchimba visima ni vyema kuzingatia ushauri wa wataalam kwa kuchimba visima virefu badala ya vifupi kwa kuwa maji ya juu yanayopatikana kwenye visima vifupi siyo salama kwa matumizi ya binadamu.

Mfanyabiashara wa Soko la Azimio mjini Tunduru Andrew John amesema ,maji hayo yatamaliza adha kubwa ya maji katika soko hilo ambalo kwa muda mrefu halina maji ya uhakika.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.