Uboreshaji wa Miundombinu ya Afya
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa fedha kiasi cha Tsh 12,854,209,081 kwa ajili ya kujenga na kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya 25 na nyumba za watumishi kwenye Halmashauri zote nane (8) za Mkoa wa Ruvuma.
Hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba hadi ya kufikia June, 2020.
Serikali ya Dkt.John Pombe Joseph Magufuli imeongeza upatikanaji wa dawa kwa kuongeza fedha kutoka Tsh 883,303,792 mwaka 2015 hadi kufikia Tshs. 4,545,139,214 mwaka 2020 ambapo upatikanaji wa dawa umeongezeka kutoka 51% mwaka 2015 hadi 96% mwaka 2020.
Mapambano dhidi ya UKIMWI
Mkoa wetu unaendelea na mapambano katika kukabiliana na tatizo la Kupunguza maambukizi ya UKIMWI ambapo hadi kufikia mwaka 2020, maambukizi ya UKIMWI yamepungua hadi kufikia 5.6% kutoka 7% mwaka 2015.
Hali ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 katika mkoa wa Ruvuma vimepungua hadi kufikia 5/1000 ukilinganishwa na vifo 12/1000 mwaka 2015. Aidha, vifo vya watoto chini ya mwaka 1 navyo vimepungua kutoka vifo 9/1000 mwaka 2015 hadi vifo 3/1000 mwaka 2020, hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika sekta ya afya.
Mkoa umeendelea kutoa chanjo kwa watoto walio chini ya miaka mitano ili kuwapatia kinga dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Hadi kufikia mwaka 2020 Mkoa wa Ruvuma umeweza kutoa chanjo kwa Watoto kwa 119% ikilinganishwa na 96% mwaka 2015. Chanjo hizo ni pamoja na chanjo ya kuzuia Kifua kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda kwa watoto wachanga, homa ya Ini na Nimonia. Haya ni mafanikio makubwa yaliyotokana na uwezekezaji mkubwa uliofanywa na Mh. Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli katika Afya kinga.
ITAENDELEA KATIKA SEKTA YA KILIMO
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.