Maelekezo ya Ilani ya CCM ya mwaka 2015 ni kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama vijijini unaongezeka toka asilimia 67.7 mwaka 2015 na kufikia asilimia 85 mwaka 2020; miji ya makao makuu ya Mikoa toka asilimia 68 mwaka 2015 kufikia asilimia 95 mwaka 2020 na miji mikuu ya Wilaya na miji midogo toka asilimia 57 hadi asilimia 90 mwaka 2020.
Hali ya huduma ya maji katika Mkoa
Katika kuboresha sekta ya maji Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Rais umetupatia Fedha kiasi cha Tshs. 16,368,911,105.11 hadi mwaka 2020 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji.
Hadi kufikia mwaka 2020 jumla ya wananchi 1,149,867 walikuwa wanapata huduma ya maji safi na salama ikiwa ni asilimia 63.9 ya wakazi wote wa Mkoa kutoka asilimia 57 ya wananchi waliokuwa wakipata huduma hii mwaka 2015.
Maji Vijijini
Wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanaopata huduma ya maji safi na salama wanakadiriwa kuwa 888,005 ambao ni sawa na asilimia 61.6 na wanapata maji kupitia vituo vya kuchotea maji 5,631. Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na kufikia malengo ya kitaifa, Mhe, Rais ameendelea kuwezesha ukarabati na ujenzi wa miradi mipya ya maji, kuanzisha na kusajili kisheria jumuiya za watumia maji vijijini kwa ajili ya kusimamia na kuendesha miradi ya maji kwani miradi hii ni ya wananchi wenyewe.
Maji mijini
Mkoa wa Ruvuma unayo miji sita ambayo ni makao makuu ya Halmashauri ukiwepo mji wa Songea ambao ni makao makuu ya Mkoa. Miji hiyo ni Songea, Mbinga, Tunduru, Namtumbo, Mbambabay na Madaba. Hadi kufikia mwaka 2020 huduma ya maji safi na salama katika Manispaa ya Songea inapatikana kwa asilimia 91 ikilinganishwa na asilimia 72.7 kwa mwaka 2015.
Mpango wa utekelezaji miradi ya maji vijijini.
Mhe. Rais katika mwaka wa fedha 2019/2020 ametupatia kiasi cha Tsh 1,168,888,500.83 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa miradi 29 ya maji.
Aidha, Mhe. Rais ametupatia Tsh bilioni 7.8 kwa ajili ya Kujenga, kukarabati na kufanya upanuzi katika miradi 33 ya maji kwa wilaya zote.
Hali ya utekelezaji wa miradi kupitia programu ya lipa kwa matokeo na Mfuko wa Maji.
Hadi kufikia mwaka 2020 Kupitia Program ya lipa kwa matokeo , Jumla ya miradi kumi na tisa (19) imekamilika na miradi kumi (10) inaendelea kutekelezwa, Miradi thelathini na tatu (33) iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.
Katika kukabiliana na tatizo la maji, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya maji na kupanua mitandao ya maji ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama. Maboresho katika sekta ya maji kama yanavyoonekana yanatokana na malengo thabiti ya Mhe. Rais ya kumtua mama ndoo Kichwani.
“MAGUFULI MAJI BOMBANI, MAGUFULI MAJI NYUMBANI”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.