Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk.Jairy Khanga anasema serikali kwa kutambua kuwa lishe ni suala la kimaendeleo hapa nchini,mapambano dhidi ya lishe duni imekuwa ni mojawapo ya maeneo ya kipaumbele katika mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano yaani 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao umelenga dira ya maendeleo ya mwaka 2025.
Akitoa taarifa kwenye mkutano wa nusu mwaka wa tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa Mkoa wa Ruvuma,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Jairy Khanga anasema Mkoa hivi sasa upo vizuri katika lishe ambapo mwaka jana katika eneo hilo Mkoa ulikuwa na asilimia 67 ambapo hivi sasa imefikia asilimia 84.
Hata hivyo Dk.Khanga anatoa rai kwa wadau katika tathimini hiyo wakiwemo wakuu wa wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma,makatibu tawala,maafisa lishe na wadau wa lishe kufahamu kuwa bado lipo tatizo la udumavu na utapiamlo ndani ya Mkoa.
“Tulivyoanza kiwango cha udumavu kitaifa tulikuwa asilimia 44.4 ,tathimini iliyofanyika mwaka 2018 Mkoa wa Ruvuma tumetoka nafasi ya asilimia 44.4 hadi kufikia asilimia 41.6 na kitaifa sisi tupo nafasi ya sita kwa kufanya vibaya kwenye udumavu na utapiamlo’’,anasisitiza.
Anasema ni vema wadau wa lishe wanapofanya tathimini kuelewa vizuri mahali Mkoa ulipo kwenye udumavu ili kila mmoja akawajibike katika eneo lake na kuondoka katika nafasi hiyo.
Kulingana na utafiti wa udumavu na utapiamlo nchini Mkoa wa Njombe unaoongoza kwa udumavu nchini kwa asilimia 53.7,ukifuatiwa na Mkoa wa Iringa ambapo kwa ujumla mikoa inayoongoza kwa uzalishaji mazao ya chakula nchini ndiyo imeathirika na udumavu nchini.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.