Matukio mbalimbali katika picha kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria ngazi ya Mkoa wa Ruvuma
Wananchi mkoani Ruvuma wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya sheria ili kupunguza migogoro ya kisheria katika jamii, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abass Ahmed , ametoa wito huo katika viwanja vya Soko Kuu, Manispaa ya Songea, ambapo maadhimisho hayo yamezinduliwa rasmi kimkoa.
Kabla ya hotuba yake, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mheshimiwa James Karayemaha, alifafanua malengo ya maadhimisho hayo, akisisitiza umuhimu wa wananchi kufahamu haki na wajibu wao kisheria.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Tanzania 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.