Hali ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 katika mkoa wa Ruvuma vimepungua hadi kufikia 5/1000 ukilinganishwa na vifo 12/1000 mwaka 2015. Aidha, vifo vya watoto chini ya mwaka 1 navyo vimepungua kutoka vifo 9/1000 mwaka 2015 hadi vifo 3/1000 mwaka 2020, hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika sekta ya afya.
Mkoa umeendelea kutoa chanjo kwa watoto walio chini ya miaka mitano ili kuwapatia kinga dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Hadi kufikia mwaka 2020 Mkoa wa Ruvuma umeweza kutoa chanjo kwa Watoto kwa 119% ikilinganishwa na 96% mwaka 2015. Chanjo hizo ni pamoja na chanjo ya kuzuia Kifua kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda kwa watoto wachanga, homa ya Ini na Nimonia. Haya ni mafanikio makubwa yaliyotokana na uwezekezaji mkubwa uliofanywa na Mh. Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli katika Afya kinga
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.