• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VIJANA 130 wahitimu mafunzo ya uuguzi Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: August 2nd, 2023

WATANZANIA  wametakiwa kuiamini Serikali yao juu uwekezaji wa Bandari  ya Dar es slaam uliofanywa  na mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) na kampuni ya DP Word.

Hayo yamesemwa  na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiuma wilayani Tunduru Daniel Malukuta,wakati wa mahafali ya 15 ya chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kiuma(KICoHAS) na mahafali ya tano tangu kuanza kwa ngazi ya stashahada na ya kwanza kwa ngazi ya stashahada ya mafunzo ya utabibu yaliyofanyika chuoni hapo.

Alisema serikali imefanya hivyo kwa nia njema kwa sababu uwekezaji huo  kati ya Serikali na kampuni ya DP Word una manufaa makubwa kwa uchumi wa nchi yetu,hivyo Watanzania tunapaswa kuunga mkono,badala ya kutumia muda mwingi kubeza mpango huo.

Alisema,hata pale wanapotaka kuikosoa Serikali ni vyema ikatumika busara na lugha rafiki badala ya kutanguliza kashifa  na maneno ya kuhudhi yanayoweza kuwagawa Watanzania.

“sasa hivi hapa nchini habari kubwa inayoendelea ni juu ya uwekezaji wa Bandari yetu uliofanywa na Serikali,kumekuwa na upotoshaji mkubwa na bahati mbaya suala hili linaonekana kushabikiwa sana,nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kuiamini serikali na hata tunapokosoa basi tutumie lugha rafiki na watu wanaoelekezwa wanasikia na watalifanyia kazi”alisema Malukuta.

Alisema,kanisa la Upendo wa Kristo Masihi-Kiuma linapenda watu wake na jamii kwa ujumla kueleza shida na maoni yao  kwa utaratibu na siyo kutumia lugha za kuhamasisha vurugu na maandamano ambayo hayana tija na afya na siyo utaratibu  katika nchi yetu.

Malukuta ameishukuru serikali kwa ushirikiano mkubwa uliotoa kwa taasisi ya Kiuma  hali iliyo wawezesha kutekeleza  masuala mbalimbali ya kiroho na kuwapatia watanzania hasa vijana elimu na stadi mbalimbali ili ziweze kuwasaidia katika kukabiliana na maisha.

Amewataka wahitimu kwenda kuwa chachu ya kuharakisha kukua kwa uchumi,kutoa mchango kwa jamii,kuwa waaminifu na waadilifu kulingana na maadili ya taaluma zao na kuonyesha umahirikatika kazi zao ili kuwa mfano wa kuigwa utakao kiletea heshima chuo hicho na taasisi ya Kiuma.

Aidha,amewaasa wahitimu hao kuepuka kujiingiza kwenye vitendo viovu vinavyokwenda kinyume na maadili na utamaduni wa nchi yetu ikiwemo  tatizo la ushoga lililoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini na Ulimwenguni.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Mariana Njeama alisema, katika mahafali ya mwaka huu jumla ya wahitimu 130 wamehitimu fani mbalimbali kati yao wahitimu wa uuguzi na ukunga ngazi ya shahada wako 73 na utabibu wa ngazi ya stashahda wako 41.

Alisema,chuo  cha Afya na Sayansi Shirikishi-Kiuma hadi sasa kimefanikiwa kutoa wana chuo(wahitimu)takribani 243 kwa ngazi ya stashahada walioanza mwaka 2019 na wanaoendelea na mafunzo yao ni 335.

Alisema,kwa ujumla ufaulu wa wanachuo ni wa hali ya juu,kwani waliomaliza mwaka jana 2022 ufaulu wao ulikuwa asilimia 99.9 kwani kati yaw ana chuo 88 aliyeshindwa kufaulu ni mmoja.

Wahitimu hao katika risala yao iliyosomwa na Sarafina Kilagwa walisema,walianza  mafunzo yao mwaka 2020 katika kada ya utabibu,uuguzi na ukunga wakiwa jumla ya wana chuo 149 kati yao kada ya uuguzi na ukunga 81 na utabibu 69.Alisema,katika mafunzo yao ya miaka mitatu wamefanikiwa kuimarisha taaluma ya chuo, kwa kupata matokeo chanya katika mitihani hususani ile ya wizara,chuo kupata maabra ya kisasa yenye vifaa vyote na kurahisisha kujifunza kwa vitendo zaidi kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.