Vijana wilayani Namtumbo wahimizwa kuchangamkia fursa katika kilimo cha tumbaku kwani soko la zao hilo la uhakika ambapo kwa msimu huu 23/24 zinahitajika tani eflu 11.
Akizungumza katika kongamano la Namtumbo Kihenge lililofanyika hivi karibuni Wilayani na Namtumbo, Meneja wa SONAMCU Ltd Mkoa wa Ruvuma Ndugu Juma Mwanga ametowa wito huo kwa vijana kulima tumbaku akisema ni kilimo chenye tija.
Amesema kwa msimu wa kilimo ulioisha wa 22/23 SONAMCU iliingia mikataba na makapuni matatu ya ununuzi wa tumbaku kwa kuwauzia tani elfu 9200 lakini kutokana na changamoto za maandalizi tani 2000 ndio zilizo zalishwa kwa maana fursa ya soko bado lipo ila uzalishaji upo chini
“Wilaya ya Namtumbo ni Wilaya pekee nchini ambayo inalima tumbaku aina tatu ambazo ni tumbaku ya moshi, hewa pamoja na mvuke mikoa mingine nane ambayo inazalisha tumbaku wao ulima aina moja lakini Namtumbo imebarikiwa aina tatu”
Hata hivyo amesema kuwa chama kikuu cha Ushirika SONAMCU Ltd kinawahakikishia soko la uhakika ambapo kuelekea msimu wa 23/24 tayari kimeshaingia mikataba ya uzalishaji na uujazi wa tani elfu 11 za tumbaku.
“Sisi kama SONAMCU tutawawezesha wakulima watakao lima tumbaku katika wilaya ya Namtumbo kwa kutoa mbegu bure na kuwakoposha mbolea, madawa pamoja na kifungashio kwa idadi ya shamba la mkulima nitoe wito kwenu wa kutafuta maeneo ya kulima kwani masoko yapo”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.