Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Elizebeth Gumbo, amekipongeza kikundi cha vijana wa Kijiji cha nguvu moja, kwa kuanza kilimo cha Mahindi na Maparachihi.
Vijana hapo walipata mkopo wa kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana ambayo ni asilimia nne ya mapato ya ndani ya Halmashauri wenye thamani ya shilingi millioni saba.
Vijana hao wameamua kuwekeza nguvu na akili kwenye kilimo ambapo wamelima shamba la hekari saba kati ya hizo hadi sasa wamelima shamba lenye ukubwa wa hekari tano ambapo zao la mahindi wamelima hekari mbili na zao la maparachichi hekari tatu.
Akizungumza na vijana hao Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ili kujikwamua kimaisha
Ngumbo amekipongeza kikundi hicho kwa namna walivyojipanga na kilimo na kuwaasa vijana, kutumia fursa ya mikopo inayotolea na Halmashauri kwa ajili ya kuendesha shughuli ambazo zinaweza kuwaletea kipato
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.