• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VITENDO vya uharibifu mazingira vinavyopoteza uoto wa asili Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 5th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed  ametahadharisha vitendo vya uharibifu wa mazingira vinageuza mazingira ya Mkoa na kupoteza uoto wake wa asili na kusababisha ukame na jangwa.

Kanali Abbas ametoa tahadhari hiyo  wakati anazungumza katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea.

Amesema kutokana na ongezeko la watu katika Mkoa na Taifa kwa ujumla,watu wengi wanatumia nishati ya kuni,mkaa na mbao kwa matumizi mbalimbali hali ambayo inachochea kuongezeka kwa kasi ya uvunaji wa mazao ya misitu,kilimo cha kuhamahama na uchomaji moto misitu.

“Hali hii husababisha kuwepo kwa mabadiliko ya tabianchi kama kuongezeka kwa joto katika uso wa nchi na kubadilika kwa kalenda na upatikanaji wa mvua,hivyo tusipobadilisha vitendo vyetu vya ukataji miti na uchomaji wa mkaa,tutageuza mazingira ya Mkoa wa Ruvuma kupoteza uoto wake wa asili’’,alisisitiza.

Hata hivyo Kanali Abbas amezihimiza Taasisi za serikali na binafsi ,vikundi vya vijana na akinamama kupanda miti kwa wingi ,kutumia nishati mbadala kama vile mabaki ya mazao ya misitu,gesi,majiko sanifu,kuchoma tofali kwa kutumia pumba za mpunga badala ya kutumia kuni.

Ameziagiza Halmashauri zote mkoani Ruvuma kusimamia kikamilifu sera,sheria ndogo na miongozo mbalimbali ya utunzaji wa mazingira na matumizi mazuri ya raslimali kwa kuhakikisha wanakuwa na vitalu vya miche ya miti na kupanda miti katika maeneo yaliyoathiriwa.

Kanali Abbas ameagiza pia kulinda vyanzo vya maji,kudhibiti uchomaji moto holela kwenye msitu na kuwawezesha wananchi kupata miche mbalimbali ya miti ya matunda,maua na miti kwa ajili ya mbao ili kukuza uchumi na kuhifadhi mazingira.

Amewaasa wananchi wazingatie umbali wa kulima toka kwenye vyanzo vya maji ambao ni mita 200 kwenye chemchem na mita 60 kwenye mito na kudhibiti kilimo cha kuhamahama ambacho hakina tija kwa kuwa kinajihusisha na uchomaji moto na ukataji wa miti.

Amekitaja chanzo kingine cha uharibufu wa mazingira ni kupitia ufugaji holela na usafirishaji wa mifugo nje ya njia zilizowekwa ambapo ameagiza kudhibiti ufugaji usiozingatia taratibu na kuhakikisha wafugaji wanafuga kulingana na ukubwa wa eneo.

Mkuu wa Mkoa pia amewaagiza watendaji kuweka  mifumo mizuri ya ukusanyaji taka katika miji na mitaa sanjari ya kukomesha matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo kwa kiwango kikubwa inasababisha uharibifu wa mazingira hasa ardhini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amesema wananchi wa Manispaa ya Songea wameadhimisha siku ya mazingira kwa kufanya usafi katika eneo la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma ,eneo la Mwengemshindo ambako wamefanya usafi eneo la hekari nne na nusu kati ya hekari tano zinazotakiwa kufanyiwa usafi.

Amesema wanatarajia wiki hii kukamilisha kufanya usafi katika eneo hilo Pamoja na kupanda miti ya matunda ambapo amesema Rais Samia ametoa mabilioni kwa ajili ya miundombinu na vifaa tiba vya hospitali hiyo.

Kila mwaka Juni 5 huadhimishwa siku ya mazingira Duniani ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni urejeshwaji wa ardhi iliyoharibika na ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame.

Vijana wahamasishaji wakiadhimisha siku ya mazingira Duniani ,maadhimisho ambayo kimkoa yamefanyika  Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.