HALMASHAURI ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamefanya kikao cha kujadili mpango mkakati waTaifa wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).
Afisa Utawi wa Jamii katika Halmashauri hiyo Shani kambuga ameeleza mwongozo ulioandaliwa kwaajili ya kufanikisha utekelezaji wa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ulioanzishwa mwaka wa fedha 2017/2018 na utekelezaji mwaka 2021/2022 hadi 2026.
“Mwongozo unaelekezwa namna ya kuunda kamati na mgawanyo wa majukumu na utendaji wa kamati za ulinzi wa wanawake na watoto kuanzia ngazi ya Taifa ,Tawala za Mikoa hadi Mamkala za Serikali za Mitaa”,amesema Kambuga.
Hata hivyo amesema kamati hiyo imefanikiwa kutoa elimu kwa jamii juu ya ukatili wa wanawake na watoto katika shule za msingi 20 na shule sita za sekondari na mikutano ya hadhara vijiji na mitaa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.