Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Ngollo Ng’waniduhu Malenya amewaamuru wafugaji na mifugo yao kuondoka mara moja na kinyume cha hapo hatua za kuwakamata na kuwafungulia mashtaka zitafuata.
Akiongea na wafugaji na wananchi wa kijiji cha Kilimasera mkuu wa wilaya ya Namtumbo alisema naamuru wafugaji na mifugo yao kuondoka katika wilaya ya Namtumbo kwa kuwa hakuna maeneo ya kuchungia mifugo hiyo
“Ninyi ni watanzania wenzetu na mnastahili kuishi popote ili mradi hamvunji sheria na kwa kuwa Namtumbo hakuna eneo la kuweka mifugo hivyo akawataka kwenda wilayani Tunduri ndiko kulikotengwa kwa ajili ya kuchunga mifugo
Malenya aliwaambia wafugaji hao kuwa wilaya ya Namtumbo ni wilaya ya kimkakati huzalisha chakula kwa wingi kutokana na ardhi yake kuwa yenye rutuba ,lakini ni wilaya ambayo inategemewa kwa kuzalisha hewa ukaa kutokana na hifadhi ya mazingira na vyanzo vya mito ambayo hiungiza maji yake kwenye bwawa la kuzalisha umeme la mwalimu Nyerere.
Hata hivyo Malenya alidai Hakuna namna lazima muondoke kwa maslahi mapana ya taifa kutokana na nyie wafugaji kuchungia mifugo kwenye hifadhi ya misitu ambayo ni vyanzo ya mito na kukata miti hovyo kwenye maeneo ya hifadhi na kuchunga mifugo kwenye maeneo ya kilimo hali inayodhoofisha ardhi ya kilimo wilayani Namtumbo.
Mohamedi Omari mkazi wa kijiji cha Kilimasera alimwambia mkuu wa wilaya huyo kuwa wafugaji hao huingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima na kulisha mifugo yao hali inayosababisha kuwepo kwa njaa kwa wananchi.
Afisa mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Paul Ambokile aliwaambia wafugaji hao kuwa tatizo la kuwataka muundoke katika wilaya ya Namtumbo ni kwa sababu ya mifugo mliyonayo lakini kama huna mifugo unaruhusiwa kubaki na kufanya shughuli za kilimo mahali popote wilayani Namtumbo kutokana na wilaya kutotenga maeneo ya kuchungia mifugo.
Wilaya ya Namtumbo inaendesha zoezi la kuwaondoa wafugaji katika maeneo yasiyorasmi ambapo kabla ya zoezi hilo mkuu wa wilaya hufanya mikutano ya hadhara kila kijiji ya kuwataka wafugaji kuondoka kwa hiari yao kabla ya kuwaondoa kwa nguvu ..
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.