Wanavikundi vya wajasiriamali na wafanyabiashara waliokidhi vigezo vya kupata mkopo wa asilimia kumi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo ya mwisho kabla ya kupokea mikopo hiyo.
Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Klasta Mlingoti, mjini Tunduru yakiwa na lengo la kuwaandaa wanufaika kwa matumizi sahihi ya mikopo ili kukuza biashara zao.
Mada zilizofundishwa zilihusisha usimamizi wa fedha, uandishi wa mipango ya biashara, mbinu mbalimbali za kibiashara, na umuhimu wa kurejesha mikopo kwa wakati.
Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii katika halmashauri hiyo, Bi. Jeceline Mganga, aliwasisitiza wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze kupata faida na kurejesha mikopo bila usumbufu.
“Unaporejesha kwa wakati, unajiongezea sifa ya kukopa zaidi,mikopo ii haina riba, hivyo ni fursa ya kipekee kwa wajasiriamali kuhakikisha inawanufaisha.”,alisema Jakline
Baada ya mafunzo, wanufaika walitakiwa kusaini mikataba ili kukamilisha hatua muhimu ya upatikanaji wa mikopo hiyo. Zoezi hilo lilisimamiwa na Mwanasheria wa Halmashauri, Bi. Mwanaharusi Chiutila.
Mikopo hii inalenga kuwawezesha wananchi wa Tunduru kujikwamua kiuchumi, kukuza biashara, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi wilayani humo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.