WAKALA wa Vipimo mkoani Ruvuma wametoa semina iliyolenga kuongeza uelewa juu ya vipimo matumizi sahihi kwa wadau mbalimbali.Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kufunguliwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema.
Akizungumza wakati anafungua Semina hiyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema amewapongeza wakala wa vipimo kwa kutoa semina hiyo iliyolenga makundi mbalimbali ikiwemo Wakulima,Wajasiliamali,Viongozi wa Masoko, Wasindikaji wa Unga,na wafanyabiaashara wa Jumla.
“Natoa shukrani zangu za pekee kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga mazingira bora ya ufanyaji wa Biashara ya Mazao na kuendelea kusisitiza utumiaji wa Vipimo sahihi ili kuleta tija na usawa kwa Mkulima ”,alisisitiza Mgema.
Hata hivyo Mgema amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Wakala wa Vipimo kutoa elimu kwa jamii kupitia Televisheni,magazeti,Radio,warsha,seminana Mikutano mbalimbali.Amesema kumekuwa na matumizi makubwa ya Vipimo batili katika maeneo ya Biashara hususani kwenye Masoko ya Manispaa na Wilaya na watu wamekuwa wakitumia Vipimo visivyo rasmi vinavyojulikana kama makopo,dumla,ndoo na lita.
Kaimu Mkuu wa Mkoa ameipongeza Taasisi ya Wakala wa Vipimo kwa kuanzisha maeneo mapya ya ukaguzi ili kupanua wigo wa kumlinda mlaji kutokana na matumizi sahihi ya Vipimo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoani Ruvuma Nyagabona Mkanjabi amesema katika Mkoa wa Ruvuma matumizi ya Vipimo sahihi yapo chini sana kwa wafanyabiashara ishara inayoonesha bado hawajahamasika kutumia vipimo sahihi.Mkanjabi amewaomba wafanyabiashara kuanza kutumia vipimo sahihi ili wananchi na serikali waweze kunufaika na vipimo sahihi.
“Mafunzo haya ni muhimu kwa sababu yatatuwezesha kuongea lugha moja ya kutumia vipimo sahihi na kuachana na vipimo ambavyo sio sahihi’’,alisema.
Stephen Ndaki ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma,amesema mafunzo haya ni muhimu kwa sababu yatawaondoa wafanyabiashara kwenye matumizi ya vipimo batili na kwenda kwenye vipimo sahihi.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Mei 5,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.