Wakandarasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wametakiwa kutekeleza miradi kwa wakati na kwamba kutofanya hivyo ni kumuhujukumu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye anatoa fedha nyingi za miradi.
Hayo yamesemwa na Afisa Utumishi katika Halmashauri hiyo Ephrem Kawonga ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji kwenye hafla ya uwekaji saini ya Utekelezaji wa Miradi Miwili baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo na Wakandarasi.
Mikataba iliyosainiwa ni Pamoja na Ujenzi wa Mradi wa Madarasa Nane (8) na Matundu kumi (10) ya vyoo katika shule ya Sekondari ya Namabengo pamoja na Ujenzi wa Madarasa matano (5) katika Shule ya Msingi Likuyusekamanga.
Kawaonga amewataka Wakandarasi Kufanya kazi Kwa kujituma na Kuendana na Muda wa mkataba.
Katika hatua hiyo Kawonga amewataka pia wakandarasi hao kufanya kazi kwa Ufanisi na Kujituma kwa kuzingatia Viwango ambavyo vimekusudiwa na Serikali ya Awamu ya
sita.
Wakandarasi waliopokea Tenda hizo na Kutia Saini ni Pamoja na Mkaka Construction ambaye amepokea Tenda ya Ujenzi wa Madarasa matano (5) katika Shule ya Msingi Likuyusekamaganga na Kampuni ya Ballpark Construction ambapo Mkandarasi amepokea Tenda ya Ujenzi wa Madarasa Nane (8) Pamoja na Vyoo Matundu kumi (10) katika shule ya Sekondari Namabengo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.