• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKULIMA kuanza kupata pensheni ya uzeeni

Imewekwa kuanzia tarehe: July 19th, 2022

WAKULIMA wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wanatarajia kuanza kupata pensheni ya uzeeni.

Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini Asangye Bangu Akizungumza na vyama vya Ushirika vya Msingi vya Ligunga,Namatili na  Mtetesi katika Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma na wakulima wa Chama cha Msingi Nanyumbu mkoani Mtwara amesema,serikali imedhamiria kuhusisha Mfumo wa stakabadhi ghalani na pensheni kwa wakulima ili wakulima waweze kumudu kuendesha maisha yao wanapokuwa wazee.

Amesema uwezo wa kufanya kazi kwa wakulima  wakiwa vijana ni tofauti na wanapofikisha miaka 60 hivyo wakulima watakaokuwa wanauza kwenye Mfumo wa stakabadhi ghalani michango yao kidogo kidogo itafanyika  kwenye mfumo ili kujiwekea pensheni uzeeni.

"Nguvu zinapokuwa zimepungua,mashamba bado unayo hivyo pensheni itawawezesha wakulima wazee kuendelea kupata fedha za kuwalipa vibarua watakaokuwa wanawafanyia kazi za kilimo",alisisitiza Bangu.

Hata hivyo amesema pensheni hiyo kwa wakulima itaunganisha na mambo mengine muhimu kwa wazee kama Bima za Afya na mikopo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,serikali ipo katika hatua za awali za kuhakikisha kuwa suala la pensheni kwa wazee linafanikiwa.

Bangu amebainisha kuwa wataalam Kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wakishirikiana na Ofisi ya stakabadhi ghalani wapita kwa wakulima  ambao watapenda kujiunga kwenye mfumo huo ili kutoa elimu ya uelewa kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Amesema licha ya kwamba pensheni kwa wakulima  ni jambo geni lakini litakuwa msaada mkubwa kwa wakulima na kwamba litaongeza hamasa kwa vijana ambao bado wana nguvu lakini baada ya miaka kadhaa watafikia uzeeni.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru TAMCU Musa Manjaule ameutaja mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa una faida nyingi kwa mkulima.

Manjaule amesema wakulima wa Tunduru walianza kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani tangu msimu wa mwaka 2015/2016 hali inayowawezesha wananchi kuendelea kupata bei nzuri ya mazao.

Amewataja mazao ambayo yapo kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani Wilaya ya Tunduru kuwa ni korosho,ufuta na mbaazi na kwamba wakulima wanafurahia mfumo huo ambao umeboresha maisha yao kwa sababu  wanalipwa kwa wakati.

"Sisi kama wakulima wa Tunduru ukituambia tusitumie mfumo wa stakabadhi ghalani hatukuelewi kwa sababu tunajua uzuri wa Mfumo wa stakabadhi ghalani na ubaya wa ununuzi wa mazao kwa mfumo holela ",alisema.

Kwa upande wake mkulima khadija Rajabu wa  kijiji cha Ligunga Wilaya ya Tunduru amesema licha ya  wakati mwingine kujitokeza changamoto ya kuchelewa kwa malipo bado mfumo wa stakabadhi ghalani ndiyo mkombozi wa mkulima kwa sababu unalinda haki ya mapato ya mkulima.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Julai 18,2023



Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.