MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Laban Thomas akiwakilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Louis Chomboko amezindua maonesho ya Nane nane.
Akizungumza katika viwanja vya nanenane Mkoani hapo Chomboko amesema Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa saba inayozalisha Mazao ya Chakula na kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo.
"Kutokana na uwingi huo wa mazao Mkoa kwa kushirikiana na wizara ya kilimo inampango wa kujenga Maghala 31 kwa ajili ya kuhifadhia Chakula yenye Jumla ya ujazo wa Tani 31 elfu ambapo kila ghala litakua naujazo wa tani elfu moja"
Chomboko ametoa rai kwa wananchi kuendelea kufuga mifugo kama kuku, Nguruwe,Mbuzi na kufanya jitihada za kuongeza mabwawa ya Samaki ili kuboresha lishe nakuongeza kipato.
Mganaga mkuu amewaomba wakulima waweze kushirikiana namabenki ili waweze kujipatia Mikopo itakayowawezesha kulima kwa tija na ufugaji bora.
Chomboko ametoa rai kwa mabenki kuweka vigezo vinavyoweza kuwaruhusu wakulima na kuwafikia pamoja na kupata elimu ya miradi pamoja na mitaji"
Chomboko amewashukuru wananchi kwa kushiriki katik Uzinduzi huo na kuwaomba washiriki katik zoezi la Sensa ya watu na namakazi ifikapo Agosti 23,2022.
Afisa kilimo wa Mkoa wa Ruvuma akimwakilisha Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Onesmo Ngao amesema maonesho hayo yanalengo la kuwawezesha wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kupata Elimu ya ili waweze kulima kwa Tija pamoja na kujifunza Teknolojia mbalimbali.
Ngao amesema maonesho hayo yatakuwa kwa mda wa siku nane na yatapelekea wakulima kupata maarifa ya kilimo pamoja na ufugaji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde na Janeth Ndunguru
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 4,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.