• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKULIMA Tunduru wamshukuru Rais kwa pembejeo za bure

Imewekwa kuanzia tarehe: July 18th, 2023

WAKULIMA wa zao la korosho katika kijiji cha Mtonya kata ya Mindu wilayani Tunduru,wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa bure pembejeo na dawa(Sulphar) za kupulizia mashamba ya korosho.

Wamesema,mpango huo uliofanywa na Rais Samia umesaidia kuhamasisha wakulima wengi kufufua  mashamba yao na kueleza kuwa utaongeza  uzalishaji wa korosho hapa wilayani Tunduru.

Stamili Yakiti,ameipongeza serikali ya awamu ya sita  kwa uamuzi wa kuweka ruzuku kwenye pembejeo za korosho kwa kuwa utachochea na kuongeza uzalishaji.

Alisema,miaka ya karibuni uzalishaji wa zao hilo ulishuka kutokana na wafanyabiashara binafsi kuuza pembejeo kwa bei kubwa hali iliyosababisha baadhi ya wakulima kushindwa kuhudumia mashamba yao.

Joseph Kalo mkulima kutoka kijiji cha Liwangula alisema,uamuzi wa Rais Samia ni mzuri na unakwenda kuleta tija kwa wakulima tofauti na miaka ya nyuma ambapo pembejeo zilizoletwa na wafanyabiashara zilikuwa chache na ziliuzwa kwa bei kubwa,hivyo kusababisha baadhi ya wakulima kutelekeza mashamba yao.

Alisema,hata mfumo wa ugawaji wa pembejeo mwaka huu ni mzuri kwani hautoi nafasi  kwa wasimamizi kuiba na wakulima wanapata pembejeo kulingana na ukubwa wa mashamba na mahitaji yao.

Hata hivyo,ameiomba serikali kuongeza kiwango cha dawa hasa Sulphar ya maji ili kukidhi mahitaji hatua itakayosaidia  kuongeza uzalishaji wa korosho mashambani kwa msimu wa kilimo 2023/2024.

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru(TAMCU Ltd)Iman Kalembo alisema,utaratibu uliotumika mwaka huu ni nzuri na wakulima wengi wana ufurahia na hadi sasa hakuna malalamiko yaliyojitokeza ambapo amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuwezesha upatikanaji wa pembejeo.

Amewashauri wakulima wa korosho kuwa,baada ya kukamilika kwa zoezi hilo kuwashirikisha maafisa ugani kwa ajili ya kufanya tathimini ya ukubwa wa mashamba yao ili waweze kupata mahitaji halisi ya pembejeo.Alisema,makisio ya uzalishaji wa korosho katika msimu wa mwaka 2023/2024 ni tani 25,000 hata hivyo uzalishaji unaweza kuongezeka kutokana na mwitikio mkubwa wa wakulima kuchukua pembejeo zilizotolewa bure na serikali zitaongeza uzalishaji wa zao hilo.

Meneja wa bodi ya korosho Tanzania tawi la Tunduru Shauri Mokiwa amewataka wakulima kutambua kuwa,ruzuku ya pembejeo ya zao la korosho inayotolewa na serikali ni mchango wake katika kumpunguzia mkulima gharama ya uzalishaji wa zao hilo.
Alisema,serikali inachangia  kwa sehemu ndogo hivyo ni muhimu kwa wakulima kujiwekea akiba ya fedha kwa ajili ya kuongeza kununua viuatilifu kwa wafanyabiashara ili waweze kutosheleza mahitaji yao.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • BODI ya kwanza ya maji yazinduliwa Tunduru

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.