WAKULIMA wa korosho waliotapeliwa fedha zao zaidi ya Sh milioni 44 na vyama vya msingi vya ushirika katika msimu wa korosho wa 2020/2021 katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameanza kurejeshewa fedha.
Akikabidhi fedha kiasi cha Sh 44.2 kwa wakulima hao,Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amesema, fedha hizo ni kati ya fedha ambazo wakulima wa korosho waliibiwa na viongozi wa vyama vya Ushirika.
Mkuu wa wilaya, ametoa siku thelathini kwa vyama vya ushirika wilayani humo kuhakikisha wanalipa fedha zilizobakia Sh milioni 11 ili kumaliza kulipa fedha zote kwa wakulima kabla ofisi yake haijaanza kuchukua hatua dhidi ya viongozi hao.
Aidha Mtatiro, amekabidhi kiasi cha Sh. milioni 18 kwa walimu wastaafu waliodhulumiwa fedha zao na Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) wilayani humo.Mtatiro ametangaza msako mkali kwa walimu wote wenye tabia ya kukopa fedha na kukabidhi kadi za Benki kwa wakopeshaji kwani kufanya hivyo ni kuidhalilisha Serikali.
“sio akili hata kidogo kadi ya benki ni mali ya benki hata mtu anayemiliki sio ya kwake ni mali ya Benki,unawezaje kumkabidhi mtu mwingine akaye na kadi yako,kwa hiyo tutaendelea kuwaelimisha walimu kuhusiana na tabia hiyo na wale watakaoonekana hawaelewi basi tutalazimika kutumia nguvu kidogo kuwaelewesha”amesema Mtatiro.
Akiongea kwa niaba ya wenzake,Mwalimu Mstaafu Juma Yasin amemshukuru Mkuu wa wilaya kutokana na jitihada anazochukua dhidi ya vyama vya akiba na mikopo ambavyo vinawadhulumu walimu na watumishi wengine wanaokwenda kukopa fedha.
Amesema, kuna walimu wengi wamekufa na wameacha fedha zao kwani hata kiasi cha Sh milioni 18 zilizokusanywa ni sehemu ndogo ya fedha walizodhulumiwa walimu wastaafu na chama hicho.
Imeandikwa na Mhidin Amri Tunduru
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.