Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inasimamia utolewaji wa masomo ya Sekondari kwa njia mbadala katika vituo na shule za sekondari wilayani Tunduru.
Serikali Katika kuhakikisha wanafunzi wa kike waliokatisha masomo yao ya sekondari katika mfumo rasmi, kwasababu mbalimbali zikiwemo ujauzito, hali ngumu ya maisha, maradhi ya kudumu na nyinginezo wanarudi shule na kuendelea na masomo yao, imeandaa program mbalimbali za Elimu ya Sekondari kwa njia mbadala (alternative Education Pathway).
Akifafanua Afisa Elimu ya watu wazima (DSAEO) wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Bi. Mariam Magulima, katika kikao maalumu cha walimu na wanafunzi, alielezea program tatu ambazo ni SEQUIP-Aep ambayo hutolewa kwa wasichana (kuanzia miaka 13-21) waliokatisha masomo yao ya Elimu ya Sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo,ujauzito, ugonjwa na hali duni ya maisha, na kwamba gharama za program hii zinatolewa na serikali.
Aidha, Bi. Mariam Magulima, alisema program ya pili ni ya masomo ya jioni (Private Candidate), walengwa ni wote waliomaliza darasa la saba (VII) lakini hakuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza, walioacha kusoma Sekondari kwa sababu mbalimbali, gharama zake zinachangiwa na wazazi/walezi (wahusika)
“Program ya tatu inawalenga wote waliomaliza elimu yao ya kidato cha nne na hawakufauru (Re-siters)” Alisema Bi. Mariam Magulima “Ninyi ambao mmefanikiwa kujiunga na program hizi mkawe mfano bora kwa wengine wenye sifa kama zenu, ili kila mmoja wetu asikose fursa ya kupata Elimu Bora”.
Vituo 8 Wilayani Tunduru vinaendelea kupokea wanafunzi ambao watajiunga na program hizi kwa mwaka wa masomo 2024, vituo hivyo ni pamoja na Nandembo, Mataka, Muhuwesi, Nakapanya, Misechela, Mlingoti TRC, Nandembo FDC, Nalasi Sekondari. Hivyo,wazazi/walezi wanahimizwa kuwapeleka watoto wao wenye sifa tajwa hapo juu ili wapate haki yao ya msingi kielimu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.