• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WALIORIPOTI kidato cha kwanza Ruvuma wafikia asilimia 80.72

Imewekwa kuanzia tarehe: February 19th, 2024

WANAFUNZI walioripoti kidato cha kwanza katika shule za sekondari mkoani Ruvuma  wamefikia asilimia 80.72 hadi kufikia Februari 16 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye ukumbi wa sekondari ya Dkt.Samia Suluhu Hassan mjini Namtumbo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa,idadi ya wanafunzi walioandikishwa elimu  Awali hadi sasa imefikia asilimia 87.8 na wanafunzi wa darasa la kwanza imefikia asilimia 99 ambapo amesema hayo ni mafanikio makubwa katika Mkoa.

Hata hivyo amesema hivi karibuni umefanyika mkutano wa wadau wa elimu Mkoa wa Ruvuma ambao ulikuwa na lengo la kufanya tathmini ya hali ya elimu katika shule za msingi na sekondari.

“Tumekubaliana kila kiongozi lazima asimamie elimu ipasavyo,hii ni kuanzia viongozi walio katika ngazi ya Mkoa,Wilaya,Kata hadi ngazi ya Kijiji,kila kiongozi atapimwa utendaji wake kwa namna atakavyosimamia elimu’’,alisisitiza RC Thomas.

Akizungumzia kuhusu udumavu,Kanali Thomas amesema ili kukabiliana na udumavu,Mkoa unahamasisha upandaji miti ya matunda shuleni na kuhakikisha lishe bora inapatikana na kwamba Mkoa umeanzisha kampeni ya kupanda miche ya matunda tarehe 19 ya kila mwezi miti inapandwa katika shule za msingi na sekondari katika Mkoa mzima.

Katika kukabiliana na kero za wananchi,Mkuu wa Mkoa amesema ameunda Kamati ya Wataaalam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi .

Amesema hadi sasa jumla ya wananchi wenye migogoro ya ardhi 106  wamewasilisha malalamiko yao ambapo wananchi 87 wamesikilizwa na kwamba hadi sasa jumla ya migogoro ya ardhi 42 imetatuliwa na kumalizika.

Ameongeza kuwa Mkoa pia umefanikiwa kutatua mgogoro wa wananchi wa vijiji vya Mkuka na Mkuani Kata ya Maguu wilayani Mbinga na wananchi wa Wilaya ya Nyasa ambapo mgogoro umetatuliwa kwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kutoa eneo la ukubwa wa hekari 450 ambazo wananchi wa Mbinga wamepewa ili wawe na mradi wa panda miti kibiashara.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameweka kila tarehe 19 ya kila mwezi kukutana na wanahabari na kutoa taarifa mbalimbali za Mkoa ili wananchi waweze kupata taarifa zinazohusu Mkoa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.