WANAFUNZI wa chuo cha afya ya Wanyama na uzalishaji Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wamepewa elimu ya magonjwa yasiyopewa kipambele ili waweze kukabiliana na magonjwa hayo.
Mratibu wa Mgonjwa hayo Daktari Betty Mbawala akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho amesema kutoa Elimu inayohusu magonjwa hayo ni muhimu kutolewa kila mahali nchini kwa kuwa watu wengi wanapata matatizo ya magonjwa yasiyopewa kipamumbe na kusababisha vifo vingi.
“Tunapotoa Elimu hiyo ya Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele inasaidia kujenga uelewa wa pamoja na namna ya kujiepusha na magonjwa hayo'',alisisitriza”.
Mbawala ameyataja Magonjwa matano katika Nchi ya Tanzania ambayo hayapewi kipaumbele ukiwemo ugonjwa wa Usubi,Matende na Mabusha,Kichocho cha tumbo,Minyoo pamoja na trakoma.
Meneja wa Chuo hicho Beata Balindile akizungumza mara baada ya wataalam wa Afya kutoa Elimu hiyo amesema na wanafunzi hao kuhakikisha wanapata dawa hizo kufuatia eneo hilo lina hatari ya kupata magonjwa hayo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.