Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Mhe. Wakili, Julius S. Mtatiro, amewakabidhi Wakuu wa vyuo vya ufundi Wilayani humo majina ya Wanafunzi ambao wanakosa sifa za kujiunga na kidato cha kwanza, cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2024 ili waweze kujiunga na vyuo vya ufundi
Makabidhiano hayo yamefanyika katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, ambacho kilihudhuriwa na Maafisa Elimu Msingi, Elimu , Afisa Elimu Sekondari na Wakuu wa vyuo vya Ufundi Nandembo (FDC),Mbesa na KIUMA.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Maafisa wa Elimu ya Sekondari na Elimu ya Msingi wamesema majina 1,874 na wanafunzi wa kujiunga na vyuo vya ufundi yamekabidhiwa, ambapo Wanafunzi 1,326 ni waliomaliza elimu ya sekondari na Wanafunzi 548 ni wa elimu ya msingi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.