• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANAFUNZI Mpitimbi Sekondari waishukuru serikali kuwajengea bweni

Imewekwa kuanzia tarehe: October 25th, 2022

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Mpitimbi Halmashauri ya wilaya Songea,wameishukuru serikali kupitia Halmashauri ya wilaya Songea kuwajengea bweni jipya na la kisasa lililo saidia kumaliza changamoto ya malazi na kupata muda wa kutosha wa kujisomea.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema kuwa,jitihada za Halmashauri ya wilaya kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwamo ujenzi wa bweni hilo na vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa kwa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa jamii na mapambano dhidi ya Covid-19 ni kielelezo cha namna serikali ya awamu ya sita inavyowajali wananchi.

Salma Abdi mwanafunzi wa kidato cha tano alisema,awali walilazimika kulala kwenye bweni dogo na chakavu ambalo halikuwa salama  kwa afya zao kutokana na sakafu yake kuwa ya udongo,hivyo kusababisha  kutokea magonjwa ya mara kwa mara.

Alisema, baada ya kupata bweni jipya  wanafunzi wa shule hiyo wataendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan aliyedhihirisha nia yake ya kumkomboa mtoto wa kike kusoma kwa bidii.

Naye mwanafunzi mwingine   Jackline Panaska,amemshukuru mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama na wananchi wa kata ya Mpitimbi, kwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa bweni hilo na miundombinu mingine ya shule ambapo nguvu zao zimesaidia kupata bweni la kisasa ambalo ni mkombozi na kuhaidi kulitumia kuongeza muda wa kujisomea ili waweze kutumiza ndoto zao.



Aidha,ameiomba serikali kupitia wakala wa maji safi na salama(Ruwasa)wilaya ya Songea, kufikisha huduma ya maji hadi bwenini ili wayatumie kufanya usafi hasa kwenye vyoo ili kuwaepusha kupata magonjwa mbalimbali.

“tunaishukuru serikali yetu na mbunge wa jimbo letu mama yetu Jenista Mhagama kwa jitihada zake,hata hivyo tunaomba  huduma ya maji safi na salama yafike bwenini kwa kuwa mazingira yetu yanahitaji maji mengi kutokana na wingi wa wanafunzi tuliopo”alisema.

Mwalimu wa ujenzi wa shule hiyo Mathew Haule alisema, walipokea jumla ya Sh.milioni 80 kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa  bweni hilo ambapo fedha zilizotumika ni Sh. milioni 79,995.561 na kubaki shilingi 4,400.

Mwalimu Mathew alisema, hatua ya  Serikali kujenga bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike imewasaidia  wanafunzi hao kupata elimu bora  na kuongezeka kwa taaluma  ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Alisema,bweni hilo limejengwa mahususi  kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wa kike wa kidato cha tano na sita kutoka katika makazi yao ili kufika shule kwa wakati   na kuwawezesha kupata muda mwingi wa kujisomea na sehemu salama ya kuishi wakiwa shuleni.

“apo awali wanafunzi walitumia bweni dogo ambalo halikuwa salama kwa afya zao  kwa kuwa chini kulikuwa na udongo,hivyo kusababisha kupata mafua mara kwa mara,tunaishukuru sana serikali kwa kujenga bweni jipya”alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Songea Neema Maghembe alisema, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 serikali imetumia  jumla ya Sh.milioni 480 kwa ajili ya kujenga mabweni 6 katika shule za sekondari.

Aidha Maghembe alieleza kuwa, mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imepanga kutumia Sh.milioni 320 kujenga mabweni mengine 4 ambapo wameshapokea Sh.milioni 160 kati ya Sh.milioni 320 kwa ajili ya kujenga mabweni 2.Mkurugenzi huyo,ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuikumbuka Halmashauri hiyo  kwa kuipa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.