• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANAFUNZI wote 27,135 waliofaulu la saba Ruvuma wapangiwa shule

Imewekwa kuanzia tarehe: December 19th, 2020


Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kuwapangia shule za sekondari watoto wote 27,135 waliofaulu mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2020.

Akizungumza kwenye kikao cha kutangaza wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2021,kilichofanyika ukumbi wa Manispaa ya Songea,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa tisa nchini iliyofanikiwa kuwapangia shule watoto wote waliofaulu.

Mndeme amesema kati ya wanafunzi waliofaulu wavulana ni 12,799 na wasichana ni 14,336 na kwamba ufaulu huo ni  sawa na asilimia 78.50 ya wanafunzi waliohitimu mwaka 2020.

Hata hivyo amesema mwaka 2019 ufaulu wa darasa la saba ulikuwa ni asilimia 83.70 hivyo mwaka huu ufaulu umeshuka kwa asilimia 5.2 ambapo mwaka jana  wanafunzi waliofaulu walikuwa 32,298 kati yao wavulana 15,236 na wasichana 17,062.

“Tuhakikishe kuwa watoto wote waliofaulu wanaripoti shule mara baada ya shule kufunguliwa Januari 2021 na wazazi watakaokiuka maelekezo haya wachukuliwe hatua,isiwepo sababu yoyote itakayomzua mwanafunzi aliyefaulu kuanza shule’’,alisisitiza Mndeme.

Mndeme pia amepiga marufuku michango ya shule inayokwenda kinyume na maelekezo yaliyotolewa na serikali kupitia waraka wa Elimu bila ada.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewapongeza viongozi na watendaji wote wa serikali kwa kufanya elimu kuwa kipaumbele cha kwanza kwa kuhakikisha kuwa miundombinu ya shule inajengwa.

“Ninaagiza mwakani kusiwepo na upungufu hata wa chumba kimoja cha darasa na samani zake,pia nazipongeza Halmashauri za Madaba na Manispaa ya Songea kuwa na ziada ya jumla ya madarasa 21’’,alisema Mndeme.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki amewaagiza maafisa elimu na wadau wote wa elimu kusimamia taaluma ili ufaulu uweze kuongezeka na kuufanya Mkoa wa Ruvuma kuwa na ufaulu wa juu.

Amezipongeza kamati za mitihani katika shule kwa kufanyakazi kubwa mwaka huu,hata hivyo ameshangazwa katika kipindi cha mitihani baadhi ya walimu na wanafunzi wao wanashindwa kujiamini.

Ndaki amesema katika utafiti mdogo uliofanyika umebaini sehemu kubwa ya wasimamizi wa taaluma shuleni hawafanyakazi yao kikamilifu ya kusimamia walimu ili waweze kutoka na matokeo mazuri.

“Ukiangalia matokeo ya mwaka 2020 utabaini kuwa ni wanafunzi wachache  waliofikia ufaulu wa daraja A,wengi wanapata C na B alama ambazo haziwezi kuwafanya watoto wetu waweze kushindana kwenda kwenye shule za bweni nje ya Mkoa wa Ruvuma’’,alisema Ndaki.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Desemba 18,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.