Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaasa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma kujiepusha kutumiwa vibaya hasa kueleka katika uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Mitaa na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2024,
Hayo amayasema wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mipango uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambacho kililenga kusikiliza maoni na mapendekezo kwa ajili ya kuchochea maendeleo na maslahi kwa umma na mkoa.
“Tunaelekea kwenye uchaguzi sitamani kuona waandishi wa habari mnatumika kwa mslahi binafsi, utakuta mtu kaandaa kikundi kwa lengo la kumchafua mtu na wewe bila kujua unaenda kuhoji kwa kumezeshwa maneno niwaombe msitumike vibaya tumieni kalamu zenu ili kulinda amani ya taifa”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.