Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imewapongeza wananchi wa Kijiji cha Malindindo kilichopo Kata ya Kambarage kwa kuchangia shilingi milioni 20 katika ujenzi wa Zahanati ambayo inatarajia kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya 2000 wa Kijiji hicho.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Maguu Mhe. Bahati Mbele wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Hii ndio ari anayoitaka Rais Samia tuendelee kumuunga mkono katika utekelezaji wa miradi mingine iliyopo na itakayokuja kwasababu sisi ndio wanufaika namba moja wa miradi hii’’,alisema.
Naye Mtendaji wa Kijiji cha Malindindo Cleopatra Lindi amebainisha pamoja na nguvu za wananchi Kijiji kilipokea milioni 50 kutoka Serikali Kuu na Zaidi ya shilingi milioni saba kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa ajili ya kumalizia mradi huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.