• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI Namtumbo waomba madini ya Urani kuanza kuchimbwa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 4th, 2023

Wananchi wa Mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo Mkoani Ruvuma wameiomba serikali mradi wa uchimbaji wa madini ya Urani katika Kijiji cha Likuyu.

Wananchi hao wametoa ombi hilo kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mheshimiwa Vitta Kawawa wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Kata ya Rwinga mjini Namtumbo.

Wananchi hao walisema mradi wa uchimbaji wa madini ya Urani katika Kijiji cha Likuyu umebaki kimya kwa muda mrefu licha ya kupewa matumaini ya kuanza Kwa mradi huo.

Shami Kingovaye mwananchi wa kata ya Rwinga ametoa rai kwa serikali kuanza kutekeleza mradi huo ambao amesema utachangia maendeleo ya wilaya ya Namtumbo na Taifa kwa ujumla.

Kingovaye amesema wananchi wa Namtumbo  wana matumaini makubwa ya kuanza Kwa mradi huo  ambao utawanufaisha wananchi kiuchumi Kwa kuuza bidhaa zao kupitia mkusanyiko wa watu watakaokuwepo wakati wa uchimbaji wa madini hayo.

Rashid John Mkazi wa Likuyu amesema wananchi wa Namtumbo hasa vijana wanatarajia kupata ajira mbalimbali kutokana na kuanza Kwa mradi huo .

Mbunge wa Namtumbo Vitta Kawawa pamoja na kuwashukuru wananchi wa kata ya Rwinga kutumia muda wao na kuhudhuria mkutano wake Ili waweze kuelezea kero zao.

Akijibu kero ya kuchelewa kuchimba madini ya Urani Mheshimiwa Kawawa alisema Kuna changamoto iliyojitokeza kati ya TANAPA na kampuni iliyopewa jukumu la kuchimba madini hayo hali iliyochelewesha mradi huo kuanza kutekelezwa.

Amesema Kampuni ya MANTRA iliyopewa jukumu la kuchimba madini hayo ilikumbana na kikwazo hicho na kusubiria utaratibu mwingine unaofanywa na Serikali  ili mradi huo uanze kutekelezwa na wananchi kuanza kunufaika.

Hata hivyo Mheshimiwa Kawawa alibainisha kuwa awali changamoto ilikuwa eneo linalotakiwa kuchimba madini hayo lipo katika hifadhi na eneo ambalo ni urithi wa Dunia( world heritage) na kwamba kulingana na Sheria za kimataifa za uhifadhi haitakiwi kufanyika shughuli yoyote ya kibinadamu bila idhini ya Mamlaka husika kwenye eneo la urithi wa Dunia.

Hata hivyo Mbunge huyo wa Namtumbo alisema  kuwa Serikali ililiondoa eneo hilo kwenye hifadhi Ili kuiwezesha Kampuni ya MANTRA iliyopewa idhini ya kuchimba madini hayo iweze kuchimba na kwamba  kampuni hiyo haikuweza kuanza mradi wa kuchimba madini hayo baada ya kushuka bei katika soko la Dunia.

 Ameeleza kuwa wakati Kampuni hiyo inasubiri bei nzuri katika soko la Dunia, Serikali iliamua eneo hilo kulitoa kwenye hifadhi kutoka hifadhi ya Taifa ya Selous Kwa wakati ule na kukitenga kipande Cha eneo kilichokuwa na madini ya Urani na kukipa jina la Undendeule forest Ili kuruhusu madini hayo yaweze kuchimbwa Kwa manufaa makubwa ya taifa.

 Amesema baada ya hifadhi kuitwa hifadhi ya Taifa ya Nyerere na kuwa chini ya TANAPA kumejitokeza changamoto tena kwa TANAPA kuhusu kutokuwa na taarifa ya uchimbaji huo wa madini katika maeneo ambayo yapo chini yao ambapo Serikali inalifanyia kazi  suala hilo na kulitafutia ufumbuzi ili wananchi waanze kunufaika na mradi huo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.