• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI Ruvuma waaswa kuchanja mbwa wao

Imewekwa kuanzia tarehe: September 13th, 2024

Na Gustaph Swai-RS Ruvuma

Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amewataka Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha Mbwa wote wanachanjwa na kufungiwa ndani mda wote wa Mchana.

Ametoa wito huo katika kilele cha  maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa duniani yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya kata ya Matarawe wilayani Songea.

"Serikali inaposisitiza kuhakikisha Mbwa wote wanachanjwa na wanafungiwa ndani mda wote wa Mchana inakusudia kuhakikisha kuwa watu wanafanya shughuli zao za maendeleo bila kikwazo cha woga wa kupata kichaa cha Mbwa au kujeruhiwa na Mbwa", alisema.

Kapenjama amewaasa wananchi kushirikiana kuhakikisha wanatoa taarifa kwa Ofisi husika wanapoona Mbwa wanazurura mchana au wanapokuwa na taarifa ya Mbwa wasio na wamiliki.

Ametoa rai kwa Wananchi kutafakari namna wanavyoshiriki katika kuthibiti ufugaji holela wa Mbwa kwani katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawataka kuwapa Mbwa huduma zote za Msingi kama Chakula, Matibabu na malazi.

Sanjari na hayo amewataka wale wanaotumia Mbwa katika shughuli za kuchunga mifugo au kuwinda kuwaweka chini ya uangalizi Mbwa wao ili wasidhuru  watu wengine.

Naye Daktari wa Mifugo Manispaa ya Songea Seria Shonyela  amebainisha kuwa Manispaa ya Songea ina Mbwa zaidi ya Elfu10 na kuwasihi wananchi kujitokeza kuchanja Mbwa wao na kupunguza Mbwa wasio na wamiliki.

Kwa upande wake Mwananchi anayemilikii  Mbwa Hendrick Mbena ameishukuru Serikali kwa kutoa chanjo ya kichaa cha Mbwa bure na kuwahimiza Wananchi wengine kujitokeza kuchanja Mbwa wao ili kuunga juhudi za Serikali za kuzuia madhara ya kichaa cha Mbwa.

Kichaa cha Mbwa ni Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Kichaa cha Mbwa na huathiri wanyama wote hususani Mbwa na binadamu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • BODI ya kwanza ya maji yazinduliwa Tunduru

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.