Wananchi, viongozi wa serikali, wanafunzi, na wakazi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameungana kuadhimisha kumbukizi ya Vita ya Majimaji kupitia mdahalo maalum ulioandaliwa na Mkoa wa Ruvuma.
Mdahalo huo uliolenga kuhimiza uhifadhi wa historia na utamaduni wa Kitanzania ulihudhuriwa na Rahel Kisusi, Mwakilishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Akizungumza katika mdahalo huo, Kisusi aliwataka wananchi kutambua kuwa Vita vya Majimaji havikuwa tu vita vya silaha, bali pia mapambano ya maadili, ujasiri, na mshikamano wa Watanzania katika kupinga ukoloni.
“Vita ya Majimaji ni sehemu muhimu ya historia yetu, na tunapaswa kuvitunza kama urithi wa taifa. Vijana wanapaswa kujifunza na kuthamini mapambano yaliyowezesha uhuru wa nchi yetu,” alisisitiza.
Aidha, aliwahimiza vijana kujifunza historia ya taifa ili kudumisha utaifa na mshikamano, akiongeza kuwa kuendeleza mila na desturi za Kitanzania ni njia bora ya kudumisha amani na umoja wa taifa.
Washiriki wa mdahalo huo walieleza kuwa kumbukizi za Vita ya Majimaji ni muhimu kwa kuimarisha uzalendo na kuhakikisha historia ya taifa inasalia hai kwa vizazi vijavyo.
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.