Mratibu wa Bima ya afya ya jamiiiliyoboreshwa Joseph Ngwenya amewataka wananchi wa Kijiji cha Mdundualo kujiunga na Mfuko wa Bima ya afya iliyoborehwa iCHF ili wasipate changamoto ya matibabu pale wanapougua.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Kijiji uliofanyika Tarehe 4 September katika Kijiji hicho ambapo katika maelezo yake amesema kwamba Bima hiyo inamanufaa makubwa sana richa ya kwamba inapatikana kwa bei nafuu.
" Bima hii inakatwa kwa TSh30,000 ikiwa na jumla ya wanachama sita kwa mwaka mzima ambapo miongoni mwa hao wanachama sita kila mmoja atachangia TSh5000 na mwanachama utaweza kutibiwa katika Zahanati kituo cha afya au hospitali yoyote ya serikali nchi nzima bila kutozwa gharama zozote ukiwa na kadi hiyo vilevile gharama hii itaambatana na upigaji wa picha kwa kila mwanachama miongoni mwa hao wanachama sita" Alisema Joseph Ngwenya.
Pamoja na hayo Joseph Ngwenya amesema kwamba sio lazima Bima hiyo itoke katika familia tu bali hata vikundi mbalimbali wanawezakuungana wanachama sita na kuweza kupata Bima Yao na ikaweza kuwasaidia.
Sambamba na hilo amewataka wananchi kutoa taarifa iwapo mwanachama yeyote amekwenda kutibiwa akiwa na Bima hiyo na kupata changamoto yoyote ili aweze kutatuliwa mara moja.
Nao wananchi wameshukuru kwa kupewa elimu hiyo kwani wanaamini kuwa kupitia Bima hiyo itaweza kuwasaidia hata wakati ambao hawatakuwa na pesa za kutosha mifukoni kwani maradhi hayachagui muda wa kuingia mwilini mwa mtu ambapo wamesema.
Felix Nditi, mwananchi " Tunawashukuru sana maafisa kwa ujio wenu katika hiki Kijiji na kutupa elimu hii ya Bima ya afya iliyoboreshwa na kupitia elimu hii naamini wengi tutajiunga kwani hii haijawahi tokea mwanzo tulikuwa tunalipa elfu10 kwa mtu mmoja lakini saivi Tumeambiwa elfu30 kwa watu sita hii itatusaidia sana sisi watu wa Hali za chini hususani katika kipindi cha kilimo Hali zinakuwa ngumu hivyo Mimi nawashauri wananchi wenzangu kujiunga na Bima hii"
Mfuko huu wa Bima ya afya iliyoboreshwa iCHF umeboreshwa toka mtu mmoja ambapo alikuwa akilipia elfu10 kwa mwaka hapo awali na sasa Bima hiyohiyo inalipiwa elfu 30 kwa watu sita huku kila mwanachama miongoni mwa hao watu sita atajipatia kadi yake ya matibabu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.