WANANCHI na viongozi wa vijiji wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma,wameonywa kutouza ardhi kwa wageni ili kupata fedha za haraka,badala yake wahakikishe wanaitunza na kuitumia kwenye shughuli za kilimo na ufugaji ili kujiletea maendeleo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mheshimia Simon Chacha,wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Nambarapi kata ya Masonya wilayani humo.
Chacha amesema,hivi sasa kumeanza tabia kwa wananchi na hata viongozi wa vijiji kuuza ardhi kwa watu wanaotoka mikoa mbalimbali hapa nchini bila kutambua kuwa huo ndiyo urithi wa watoto wao na vizazi vyao.
Ameonya,kama wananchi wataendelea na tabia hiyo kuna hatari kubwa miaka ijayo kuwa watumwa kwa kukosa maeneo kwa ajili ya kufanya shughuli zao za uzalishaji mali na kwenda kulalamika kwa viongozi ilihali walikuwa na maeneo mengi.
“mara kwa mara nitakuwa mkali sana juu ya suala la kuuza ardhi holela katika wilaya yetu,kumekuwa na tabia isiyopendeza baadhi ya wananchi kwa kushirikiana na viongozi waliopo wa vijiji kuuza maeneo kwa wageni wanaonunua ardhi kwa bei ndogo,jambo hili sitolivumilia na nitakuwa mkali kweli”alisema Chacha.
Amesema,wilaya ya Tunduru inapakana na nchi jirani ya Msumbiji,hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini kwa kutouza ardhi kwa mtu asiyekuwa raia wa Tanzania kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999,inatakaza mtu asiye raia wa Tanzania kumilikishwa ardhi kama siyo mwekezaji na mtu yoyote aliyeingia hapa nchini kwa njia isiyo stahili.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.