WAKAZI wa mikoa kumi ya kusini wamenufaika na fursa ya maonesho ya Utalii karibu kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani Iringa kuanzia Septemba 23 hadi 28 mwaka huu.
, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amesema kwenye maonesho hayo zimeoneshwa fursa za Uwekezaji na utalii kutoka kwenye mikoa hiyo.
Pia limefanyika kongamano la uwekezaji, utalii wa mitaani na tamasha ya utamaduni katika mikoa yote 10.
Shughuli nyingine zilizofanyika kwenye tamasha hilo amezitaja kuwa ni mbio za marathoni za hiari, kilomita 5 na kilomita 10, mbio za magari na pikipiki na maonesho ya wanyama hai, utalii wa kamba na burudani.
“Lengo la maonesho hayo ni kuendeleza kampeni ya The Royar Tour ilioanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na kutangaza fursa za utalii na uwekezaji zilizopo kusini mwa Tanzania,”alisisitiza RC Halima
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.