WAKAZI wa kata ya Litumbandyosi Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma,wameondokana na adha ya kutembea umbali wa kilometa 85 kufuata huduma za afya Mbinga mjini baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya Litumbandyosi kilichogharimu Sh.milioni 500.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Dkt Seleman Jumbe amesema,kituo hicho kimejengwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ni kinahudumia zaidi ya wakazi 15,000 wa kata ya Litumbandyosi na maeneo ya jirani.
Dkt Jumbe ametaja majengo yaliyojengwa katika kituo hicho ni jengo la wagonjwa wa nje(OPD)maabara,wodi ya wazazi kwa ajili ya kulaza na kujifungua,jengo la kufulia nguo,kichomea taka na kufunga jenereta.
“Sisi kama Halmashauri ya wilaya Mbinga tunaishukuru Serikali,wananchi wa kata ya Litumbandyosi na vijiji vya jirani wamepata msaada mkubwa kwa kuwepo kwa kituo hiki kwani kimesaidia wananchi kutoangaika tena kwa kwenda maeneo ya mbali kufuata huduma za matibabu”alisema Dkt Jumbe.
Kwa mujibu wa Dkt Jumbe,tangu kituo kilipofunguliwa mwezi mei mwaka huu kimesaidia sana kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto kwani hapo awali baadhi ya mama hao walipoteza maisha njiani kabla ya kufika kwenye maeneo ya kutolea huduma za afya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.