• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI wa Namtumbo kunufaika na mradi wa maji wa bilioni mbili

Imewekwa kuanzia tarehe: June 29th, 2020

WANANCHI WA NAMTUMBO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA BILIONI MBILI

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imetoa zaidi ya sh.bilioni mbili kutekeleza mradi wa maji wa Mkongogulioni na Nakahimba Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo David Mkondya akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme,amesema mradi huo ulisainiwa  Juni 12 mwaka 2013 na utekelezaji wake ulianza mwaka 2017 na ulitarajiwa kukamilika Februari 2020 chini ya Mkandarasi Kipera Contractors.

Mkondya amesema mradi huo unatarajia kuhudumia watu zaidi ya 8000 katika vijiji vya Mkongogulioni na Nahimba na kwamba kazi ambazo zimepangwa kufanyika kwenye mradi huo ni ujenzi wa tanki la lita 25,000 katika kijiji cha Nahimba na ukarabati wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 150,000 katika kijiji cha Mkongo.

Hata hivyo amezitaja kazi ambazo zimefanyika kulingana na mkataba kuwa ni uchimbaji wa mtaro katika kijiji cha Nakahimba ambao umefikia zaidi ya asilimia 83,ujenzi na ukarabati wa matanki ya kuhifadhia maji,ujenzi wa chanzo,ulazaji wa mabomba na ujenzi wa vituo 46 vya kuchotea maji.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ameridhishwa na mradi huo na kusisitiza kuwa serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 30 kutekeleza miradi ya maji katika Mkoa wa Ruvuma.

Amewaasa wananchi hao kuhakikisha kuwa wanalinda miundombinu ya maji na kutochoma moto au kuharibu kwenye vyanzo vya maji ili maji yaweze kutumika kwa muda mrefu bila kuwa na maji ya mgawo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 28,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • BODI ya kwanza ya maji yazinduliwa Tunduru

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.