BAADHI ya wakazi wa kata ya Mbinga Mhalule wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,wameupongeza wakala wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA),kwa kutekeleza vizuri ujenzi wa mradi wa barabara ya Matomondo-Mlale Jkt kwa kiwango cha lami.
Wamesema,TARURA ni mfano bora na kuigwa kwa taasisi nyingine za umma katika kutekeleza na kusimamia miradi yake,na kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,kutatua kero ya mawasiliano kwa wakazi wa kata hiyo na makao makuu ya wilaya Songea mjini.
Clous Mpenda alisema,kujengwa kwa Barabara ya Matomondo-Mlale Jkt kwa kiwango cha lami itachochea kukua kwa uchumi wao kwa kusafirisha mazao wanayozalisha na kufanya shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato kati ya Mbinga Mhalule na maeneo mengine.
Alisema kabla ya kujengwa kwa kiwango cha lami,changamoto kubwa ilikuwa namna ya kusafirisha mazao kutoka shambani kwenda sokoni kutokana na ubovu wa barabara hiyo, jambo lililochangia umaskini mkubwa licha ya jitihada kubwa wanazofanya kujikwamua na umaskini kupitia shughuli zao za kilimo.
“kwanza tunaishukuru sana serikali kupitia Rais wetu mpendwa Dk Samia Suluhu Hassan kutoa fedha zinazotumika kujenga barabara hii,pia tunawapongea wataalam wote wa Tarura kwa usimamizi mzuri,hii barabara ni muhimu sana kwetu sisi”alisema Mpenda.
Mpenda ameiomba serikali,kuendelea kujenga kipande cha barabara kilichobaki kwa kiwango cha lami ili kurahisisha mawasiliano kati ya kata ya Mbinga Mhalule-Magaguru na maeneo mengine ya wilaya ya Songea ambayo ni maarufu kwa kilimo cha zao la mahindi.
Christian Komba alisema,atatumia fursa ya barabara ya lami kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kuwaomba wananchi wenzake kuitunza barabara hiyo na kuitumia kuondokana na umaskini.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Songea Mhandisi Bakari John alisema,ujenzi wa wa barabara ya Matomondo-Mlale Jkt yenye kilomita 21 kwa kiwango cha lami ulianza mwezi April mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Machi 20233.
Alisema,barabara hiyo inajengwa kwa awamu mbili,na katika awamu ya kwanza imetekelezwa umbali wa kilomita 3.5 kwa gharama ya shilingi bilioni 4.
Alitaja kazi zilizofanyika katika awamu ya kwanza ni ujenzi wa lami kilomita 3.5,ujenzi wa madaraja makubwa 3,kujenga vivuko vidogo vya maji (makalavati)49,kujenga mifereji kilomita 2.5 na kufunga taa za barabarani.
Alisema,barabara hiyo ikikamilika itawasaidia wananchi wa vijiji vya Matomondo,Mlale,Magagura,Nakahegwa ambavyo ni maarufu kwa kilimo cha mahindi kusafirisha mazao yao na bidhaa nyingine kwa urahisi.
Mhandisi Bakari,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ambazo zimesaidia kujengwa kwa barabara hiyo na kueleza kuwa, fedha zilizotumika zinatokana na tozo ya mafuta ambapo amewataka wananchi kuitunza ili iweze kudumu kwa mrefu.
Aidha alisema,Tarura inatekeleza mradi mwingine wa barabara ya Tunduru-Janction-Seedfarm-Kuchile kutoka kiwango cha changarawe kuwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 742 zilizotolewa na serikali kuu kupitia mfuko wa barabara.
Alisema,barabara hiyo inajengwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza imejengwa urefu wa mita 800 na awamu ya pili mita 700 hivyo kufanya matengenezo ya barabara hiyo kuwa kilomita 1.5.
Alisema,barabara hiyo ni muhimu kwani inaungana na barabara kuu mbili ya Songea-Njombe na Songea-Tunduru zinazotoka nje ya mkoa wa Ruvuma,na itakapokamilika itawasaidia wananchi wa kata ya Msamala na Seedfarm kusafiri kwa urahisi badala ya kuzunguka hadi katikati ya mji wa Songea.
Alisema,ujenzi wa barabara ya Tunduru-Janction-Seedfarm-Kuchile utaendelea kutekelezwa kadri serikali itakapopata fedha kwani lengo la serikali kupitia Tarura kuijenga barabara yote kwa kiwango cha lami ili kurahisisha usafiri na mawasiliano kwa wakazi wa mji wa Songea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.