Mkuu wa wilaya ya Songea, Mhe. Pololet Mgema, amewataka wananchi ambao hawakufikiwa na makarani wa Sensa ya watu na makazi, watoe taarifa ili waweze kuhesabiwa.
Aliyasema hayo katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea alipokuwa akitaja takwimu za zoezi la kuhesabu anwani za makazi katika halmsahauri hiyo
Mhe. Mgema alisema kuwa mpaka sasa halmashauri hiyo imesajili makazi Zaidi ya 43,978. Pia alisema wale ambao hawakuweza kufikiwa na makarani kipindi cha sensa ya watu na makazi kwasababu mbalimbali watoe taarifa ili kuhisaidia serikali ipate taarifa sahihi
“Niwaombe nitumie nafasi hii kuwaeleza wananchi kuwa zoezi la kuandikisha anwani za makazi ni endelevu, lakini kama kuna mwananchi ajahesabiwa, bado ajachelewa atoe taarifa ili aweze kufikiwa na makarani na ahesabiwe kwa kufanya hivyo atakuwa ametimiza wajibu wake kisheria”alisema Mgema.
Pia ameipongeza halmashauri hiyo kwa kufanya vizuri kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuvuka malengo iliyojiwekea na kwa kufanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato na kuingia kwenye halmashauri tano bora kitaifa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.