• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANAWAKE 6,500 hufariki kila mwaka kutokana na saratani ya mlango wa kizazi

Imewekwa kuanzia tarehe: April 24th, 2024

Na Albano Midelo,Songea

WANAWAKE Zaidi ya 9,500 kati ya 100,000 hugundulika kila mwaka kuwa na tatizo la saratani ya mlango wa kizazi,kati yao wanawake 6,500 hufariki dunia kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis  Chomboko wakati anatoa taarifa ya maadhimisho ya wiki ya chanjo na uzinduzi wa dozi moja ya chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV)  kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Dr.Chomboko amesema inakadiriwa wanawake Zaidi ya 450,000 wamethibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi duniani na wengi wao wapo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

“Saratani ya mlango wa kizazi inashika nafasi ya pili kwa kusababisha saratani kwa wanawake ulimwenguni,nafasi ya kwanza inashikwa na saratani ya matiti’’,alisisitiza.

Hata hivyo Dr.Chomboko amesema hapa nchini saratani ya mlango wa kizazi inaongoza  miongoni mwa saratani zote zinazogundulika miongoni mwa wanawake wenye umri  wa kuanzia miaka 15 hadi 44.

Ameyataja mambo yanayochochea kupata saratani  ya mlango wa kizazi kuwa ni kuanza kujamiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,kuwa na ndoa za mitaala,uvutaji sigara,kuwa na mpenzi asiyetahiriwa na virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Amezitaja dalili za saratani ya mlango wa kizazi kuwa ni kutokwa damu bila mpangilio,maumivu ya mgongo,kuchoka,kutoka uchafu kwenye uke, kuishiwa damu,figo kushindwa kufanya kazi, uvumbe wa tezi na kupatwa na fistula.

Baadhi ya wadau wa maendeleo mkoani Ruvuma wakiwa kwenye maadhimizo ya uzinduzi wa wiki ya chanjo mkoani Ruvuma

Ili kujikinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi,Mganga Mkuu huyo wa Mkoa wa Ruvuma amesema ni vema kupata chanjo ya kuzuia saratani hiyo,kubadili tabia,kuepuka ngono katika umri mdogo,kuepuka uvutaji sigara na kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu.

Akizungumzia huduma za kupima na kutibu saratani ya mlango wa kizazi katika Mkoa wa Ruvuma,Dr.Chomboko amesema Mkoa una jumla ya vituo 59 vinavyotoa huduma ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi na kwamba kati ya hivyo vituo 30 vina mashine za matibabu ya saratani ya mlango wa kizazi.

Amesema katika mwaka 2023,jumla ya wanawake 13,825 walichunguzwa na kati yao wanawake 348 waligundulika kuwa na viashiria vya awali vya saratani ya mlango wa kizazi na kwamba wanawake 313 walipatiwa tiba na wanawake 119 walihisiwa kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.

Hata hivyo amesema wanawake 70 walithibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi ambao walipata rufaa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akizungumza kabla ya kuzindua maadhimisho hayo amesema Mkoa wa Ruvuma unatarajia kutoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi  kwa wasichana wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi 14 wapatao 147,447.

Ameitaja kaulimbiu ya wiki ya chanjo mwaka 2024 kuwa ni Jamii iliyopata chanjo yenye afya  ambapo ametoa rai kwa jamii nzima  kuhakikisha walengwa  wote wanapata fursa ya kupata chanjo hiyo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge ametoa rai kwa viongozi wa dini na watendaji katika ngazi zote kuendelea kuwahamasisha wazazi na walezi wenye Watoto walengwa ambao bado hawajapata chanjo hiyo kuhakikisha Watoto wao wanapata chanjo hiyo muhimu.

Chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi mkoani Ruvuma imeanza kutolewa kuanzia Aprili 22 na inatarajia kukamilika Aprili 28 mwaka huu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.