JUMLA ya watahiniwa 4,521 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita 2024 mkoani Ruvuma ambao umeanza Mei 6,2024 na unatarajia kukamilika Mei 24 mwaka huu.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Mwl. Edith Mpinzile amesema kati ya watahiniwa hao watahiniwa wa shule ni 4,313 na watahiniwa wa kujitegemea ni 208.
Amewataja watahiniwa wa Ualimu waliosajiriwa na na kufanya mtihani wa Ualimu ni 187 ambao wanatoka katika vyuo vya ualimu Songea na chuo cha Ualimu Nazareti kilichopo Mbinga.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed anawatakiwa watahiniwa wote wa Mkoa wa Ruvuma mtihani mwema wa kidato cha sita 2024 na ualimu.
Nchini Tanzania Jumla ya watahiniwa 113,504 wa kidato cha sita na ualimu ngazi ya cheti na stashahada wanafanya mitihani yao kuanzia Mei 6 hadi 24 mwaka huu .
Mtihani huo wa kidato cha sita unafanyika katika shule 931 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 258.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.