Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekamilisha safu ya uongozi ngazi ya Mkoa baada ya kuwaapisha makatibu Tawala wa mikoa tayari kwa kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia watanzania kwenye mikoa yao na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwenye maeneo yao.Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo imepata viongozi watakaosukuma mbele gurudumu la maendeleo kuanzia ngazi ya Mkoa hadi kitongoji.
Mkuu wetu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Augustine Ibuge kwa kushirikiana na Katibu Tawala wetu wa Mkoa Ndugu Stephen Mashauri Ndaki wapo tayari kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.Jambo la muhimu ni kwa watumishi wote na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano katika sekta zote ili iwe rahisi kwa viongozi hao kuwatumikia watanzania wa Mkoa wa Ruvuma katika serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Mashauri Ndaki akiwa ofisini kwake mjini Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.